Member
wa Young Money Drake Dreezy amelionja joto la hasara ya teknolojia ya
karne hii ya 21 baada ya album yake iliyosubiriwa kwa hamu na mashabiki
wake ‘Nothing was the same’ kuvuja na kupatikana kwenye mitandao siku
tisa kabla ya tarehe rasmi ya kuiachia.
Album hiyo ilitarajiwa kuingia sokoni rasmi (September 24) lakini kwa
bahati mbaya imeanza kuonekana kwenye mtandao September 15.
‘Nothing was the same’ imevuja ikiwa ni siku chache zimepita toka
Drake awasikilizishe fans wake wimbo ulioko kwenye album hiyo unaoitwa
‘Too much’ kwa kuuimba live, huku akiwa ameachia rasmi wimbo ‘Wu-Tang
Forever’ ambao ameufanya kwa kuwapa heshima Members wa kundi la Wu-Tang
Clan la New York, Marekani.
Katika album hiyo Drake amewapa shavu wasanii wakali akiwemo Jay Z,
Sampha, 2Chainz, Big Sean, Jhene Aiko, Detail na Majid Jordan.
Post a Comment