
Mlimbwende
Happiness Watimanywa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende
wenzake 30 na kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013 na kupata nafasi
ya kwanza kabisa kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo.
Shindano
hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao
ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya
shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao. Miongoni mwa mataji
hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania
Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano
la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu
ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa masuala ya urembo
Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za
warembo hao.
Taji la Redd's Miss Tanzania Photogenic linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012.
Mrembo
huyo ambaye pia anashikilia taji la Miss Dodoma 2013 na Miss Kanda ya
Kati 2013, ana digrii ya Biashara aliyoipata kupitia chuo cha
Strathclyde University cha UK na aliwahi kuwa wa kwanza na kuongoza nchi
zipatazo 150 katika somo la Accounts kwa shule zinazofanya mtandao wa
IGCSE, Happiness alikuwa akisoma katika shule ya Saint Constantines
International School ya Arusha. Alivumbuliwa na kipindi maarufu cha
wanafunzi SKONGA kinachooneshwa kupitia televisheni ya EATV na kuwa
mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengi nchini Tanzania na kwingineko.
Post a Comment