Kaimu
 Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Kufuata Kanuni za Kiislamu 
(Islamic Banking), wa Benki ya NBC Tanzania, Yassir Masoud (katikati) 
akizungumza katika droo ya awamu ya pili  kupata washindi wawili 
waliojishindia safari wao na wenza wao inayolipiwa kila kitu na NBC 
kushiriki ibada ya Hija mjini Makka nchini Saudi Arabia baadae Mwezi 
ujao. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, 
Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi
 ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
  Meneja
 Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Eddie Mhina akipiga simu 
kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya Islamic Banking ya benki hiyo ambayo
 washindi wawili na wenzao wao watalipiwa gharama zote kwenda Makka 
nchini Saudi Arabia kushiriki ibada ya Hijja baadae mwezi ujao. Wengine 
kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo, 
Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud na Mkaguzi 
Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi 
Abdulhussein.
Mkaguzi
 Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi 
Abdulhussein (katikati) akihakiki majina ya washindi wa kampeni hiyo. 
Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata 
kanuni za Kiislamu wa NBC, Yassir Masoud na Meneja Uhusiano wa benki 
hiyo, Eddie Mhina pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria 
hafla hiyo. 
Kaimu
 Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akifurahi 
pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati baadhi ya washindi 
wakielezea furaha yao baada ya kupigiwa simu na kujulishwa kujishindia 
safari ya kwenda hijja itakayolipiwa kila kitu na NBC. Kutoka kushoto ni
 Ofisa katika Idara ya Operesheni, Edesia Kahyarara, Meneja Masoko, 
Alina Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano, Eddie Mhina na  Mkaguzi Mwandamizi
 wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
Post a Comment