Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita
Rais wa Mali amesema kwamba, mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa kwa
ajili ya kutatua migogoro ya maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo yataanza
hivi karibuni.
Ibrahim Boubacar Keita amesema hayo katika kikao cha kwanza na Baraza la
Mawaziri na kusisitiza kuwa, ni jukumu la serikali kutatua kikamilifu
migogoro ya maeneo ya kaskazini na kuimarisha amani ya muda mrefu chini
ya msingi wa kuaminiana makabila tofauti ya nchi hiyo.
Rais wa Mali Septemba 4 wakati alipoapishwa ili kuanza kuiongoza nchi
hiyo pia alisema kwamba, miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele na
serikali yake ni kuanzisha mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa.
Wakati huo huo Waziri mpya wa Madini wa Mali amesema kuwa serikali ya
nchi hiyo itaangalia upya makubaliano ya madini na kuanza kuzungumza
tena na mashirika ya kigeni kujadili mikataba ambayo haina maslahi na
taifa.
Post a Comment