
Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilisihi Jimbo la Kiembe Samaki (CCM)
Mansour Yussuf Himid amesema licha ya kufukuzwa Uanachama katika chama
hicho hatoenda Mahakamani kutetea nafasi hiyo kwani kufanya hivyo ni
kukaribisha Malumbano ambayo hayana tija.
Amesema kwenda kupinga uamuzi huo Mahakamani ni kuhalalisha yeye kuwa
Mwakilishi wa Mahakama badala ya Wananchi jambo ambalo hapendelei
kutokea katika maisha yake.
Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Amesema amekuwa akiulizwa Maswali mengi na Watu tofauti kuhusu
mustakabali wake kisiasa baada ya kufukuzwa uanachama na kuongeza kuwa
hana Pesa za kuchezea kwenda kupinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi
Mahakamani.Kusoma zaidi bofya
“Wenzangu wamenipima na wameniona sifai ni haki yao, siendi
Mahakamani, sina pesa za kuchezea wala sitaki kuwa Mwakilishi wa
Mahakama” Alisema Mansour.
Mansour aliyejiunga CCM mwaka 1987 alienguliwa Uanachama siku za
karibuni kutokana na Kamati kuu ya Chama CC kuridhika na madai ya kwenda
kinyume na misimamo ya Chama pamoja na kushindwa kuitetea Ilani ya
Chama cha Mapinduzi.
Mansour ameongeza kuwa kwenda Mahakamani ni kukaribisha malumbano na
kusisitiza kuwa Waungwana hawalumbani hivyo ameamua kukaa pembeni.
Amedai kwamba baada ya kufukuzwa uanachama CCM vyama tofauti nchini
vimejitokeza kuzungumza naye ili ajiunge navyo na kudokeza kuwa bado
hajaamua ni Chama gani ataenda hadi pale muda utakapofika kufanya hivyo.
Mansour amesisitiza kuwa hata kama Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC
itaitisha uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kiembesamaki yeye hatogombea na
kwamba anaweza kufanya hivyo ifikapo mwaka 2015.
Ametumia fursa hiyo pia kuwaomba Radhi wana Jimbo la Kiembe
Samaki alilokuwa akiliongoza toka 2005 na kuwashukuru Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliomsaidia katika kupindi chake chote cha Uongozi.
Samaki alilokuwa akiliongoza toka 2005 na kuwashukuru Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliomsaidia katika kupindi chake chote cha Uongozi.
Akigusia suala la Muungano Mansour amesema ataendelea na
harakati zake kusimamia maslahi ya Zanzibar ili kuona mchakato wa Katiba Mpya unakuja na Katiba yenye Muundo wa Muungano wa Haki na Usawa baina ya Tanganyika na Zanzibar.
harakati zake kusimamia maslahi ya Zanzibar ili kuona mchakato wa Katiba Mpya unakuja na Katiba yenye Muundo wa Muungano wa Haki na Usawa baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Awali katika Kongamano hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano
Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo alimshukuru Rais Kikwete kwa ujasiri wa
kuleta mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza kuwa Kamati yake
itaendelea kudai Muungano wa usawa na haki.
Mzee Moyo amedai kuwa Kamati yake haihitaji kutambuliwa na Watu
wengine na kwamba inatosha kujulikana na Wananchi ambao wanafahamu
wajibu wa Kamati hiyo.
Itakumbukwa kwamba kabla ya Kongamano hilo Chama cha Mapinduzi
kilitoa taarifa kwa Vyombo vya habari kuhusu kutoitambua Kamati hiyo
inayoongozwa na Mzee Moyo akisaidiwa na Makamo wake Aboubakar Khamis
Bakar.
Katika hatua nyingine Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye alikuwa pia
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi Eddy Riyami alitangaza kujiengua na
Chama hicho na kusema kwa sasa yupo huru bila Chama chochote.
Kabla ya Kongamano hilo Kamati hiyo pia iliwasilisha maoni yake kwa
Tume ya Katiba mpya ambapo maoni yake yalijikita katika kuifanya
Zanzibar kuwa na Mamlaka yake kamili ndani ya Mfumo wa Muungano.
CHANZO:MAELEZO ZANZIBAR
Post a Comment