Afisa
Mwandamizi wa manunuzi Bodi ya michezo ya kubahatisha, Sadick Kasuhya
kulia akimkabidhi mmoja ya madawati 100 yaliyotolewa kwa ufadhili wa
Bodi ya michezo ya kubahatisha kwa Mbunge wa Viti maaluma kupitia chama
cha mapinduzi mkoa wa Iringa Lita Kabati tukio lililofanyika katika
shule ya msingi Sabasaba mkoani Iringa.
Na Denis Mlowe,Iringa .
MBUNGE
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa(CCM) Lita Kabati ametoa msaada wa
madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 6.3 kwa shule za msingi
zilizoko mkoani hapa.
Kabati
akizungumza wakati akikabidhiwa madawati hayo kwa ufadhili wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania mwishoni mwa wiki, alisema shule nyingi
mkoani hapa zina upungufu mkubwa wa madawati hivyo ni jukumu la kiongozi
kuweza kusaidia kuondokana na hali hii na kuwashukuru bodi ya michezo
ya kubahatisha Tanzania
“Nimefanya
ziara katika shule za msingi nyingi za mkoani kwangu kuna matatizo
mengi kama ukosefu wa madawati na vitabu ndipo nikawaomba wenzetu wa
bodi ya michezo kubahatisha wanisaidie madawati kwa shule hizi hakika
ninawashukuru sana hakika haitamaliza tatizo lakini itasaidia kupunguza
japo kwa uchache” alisema Kabati
Alisema
kuwa elimu bora kwa wanafunzi wa shule za msingi unaendana na vifaa
wanavyotumia katika kupata elimu ya msingi ikiwemo kakaa katika madawati
bora kunachangia maendeleo ya taifa letu katika kukuza elimu.
Kabati
aliwataka viongozi wengine kuondokana na tabia ya kufikiria kuwa katika
kuleta maendeleo ya mkoa ni mojawapo ya kampeni bali ni kuungana na
kuweza kupambana katika kuwaletea maendeleo wananchi wanaowawakilisha.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi madawati hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa bodi ya
michezo ya kubahatisha Tanzania, Afisa Mwandamizi wa manunuzi Bodi ya
michezo ya kubahatisha, Sadick Kasuhya alisema moja ya majukumu ya bodi
kuweza kusaidia jamii katika sekta ya elimu na wataendelea kusaidia
shule mbalimbali nchini.
Alisema
kuwa kwa msaada huu wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni
6, 3 kutasaidia kupunguza tatizo la madawati kwa baadhi ya shule
zitakazokabidhiwa msaada huo
Post a Comment