
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa
Samwel Manyere akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
zawadi ya kitini na CD vya somo la Kemia kwa wanafunzi wa shule za
Sekondari Mkoani Rukwa katika hafla fupi alipoongea na waalim wakuu wa
shule za Sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 17 Septemba
2013 katika ukumbi wa RDC mkoani Rukwa. Alisema kuwa kwa sasa kuna
umuhimu mkubwa wa wanafunzi kuhamasishwa kusoma masomo sayansi na
kuelimishwa zaidi juu ya matumizi sahihi ya tindikali tofauti na hivi
sasa inavyotumika kama silaha ya kuwadhuru watu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya akionyesha CD na kitini alichokabidhiwa na Mkemia Mkuu wa
Serikali kwa ajii ya kuvisambaza katika shule za Sekondari Mkoani Rukwa.
Mkemia Mkuu wa Serikali alisema hiyo ni sehamu ya Mpango wa Ofisi yake
na Serikali kuboresha somo la Kemia hapa nchini. Kushoto ni Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Chima.


Profesa akutana na Mwalimu wake:
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akiwa katika picha ya
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na mwalimu wake
Ndugu John Maufi aliowahi kumfundisha katika shule ya Sekondari
Kantalamba Mkoani Rukwa. Mkemia Mkuu wa Serikali aliwahi kuwa mwanafunzi
bora wa somo la sayansi hapa nchini mnamo mwaka 1987. Kwasasa
Mwalim Maufi ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Theresia ya
Mkoani Rukwa.

Post a Comment