Ben
Komba, Pwani.
Mkuu wa Mkoa
wa Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA amekemea tabia ya watendaji kusababisha migogoro
ya ardhi katika jamii kutokana na utendaji wao kuongozwa na maslahi binafsi
hali ambayo inatishia hali ya ulinzi na usalama nchini.
BIBI.MAHIZA
amewaambia watendaji katika kikao cha kuhimiza maendeleo ya Mkoa wa Pwani kilichofanyika mjini Kibaha kuwa
wanachoponzwa nacho ni tamaa ya vifedha vidogo vidogo wanavyopokea ndio kichocheo cha
uvinjifu wa amani katika wilaya, Kata na Mitaa/vijiji.
BIBI.MAHIZA
ameonya kuwa iwapo atabaini viongozi ndio wanahusika katika kuchonganisha raia,
basi atahakikisha mhusika anachukuliwa hatua za kisheria bila kujali yeye ni
chama gani au ni nani ili kuendeleza utamaduni wa kutii sheria bila shuruti.
Amewachukulia
watu wanaowachonganisha wananchi katika masuala ni wabaya ambao wanasababisha
uvinjifu wa amani.
Akiongea
katika kikao hicho Mwenyekiti wa serikali Mkoani A, BW.TITUS SAFIEL KABORA amesema kuna mambo
ambayo jamii inayaibua lakini yamekuwa hayapewi kipaumbele, akitoa mfano kwa
mtaa wake ambao umeibua barabara sugu tano ambazo walitaka zifunguliwe lakini
mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
BW.KABORA
ameeleza kuhusu suala la ujenzi holela ambao umeibuka katika mtaa wa BLOCK B na
kupewa nguvu na viongozi wa kisiasa na malalamiko yanapopelekwa hatua za
nyingine, kuna kuwa hakuna majibu na kuacha sheria zikikiukwa.
Post a Comment