Na Rehema Matowo, Mwananchi
Kuna mikasa mbalimbali huwatokea watu katika
suala zima la mapenzi, kiasi cha kusababisha baadhi yao kutopenda tena
kuingia kwenye jambo hilo wakiliona kama ni kitu kisichofaa, ingawa
ukweli unaweza kuwa sio huo.
“Sitaki tena wanaume, ni watu wabaya, wameniumiza
moyo wangu mno,” anasema Hawa Francis, mkazi wa Ubungo, Dar es Salaam.
Sababu kubwa ni kero ambazo amewahi kuzipata katika suala zima la
uhusiano. Vivyo hivyo wapo wanaume hawataki kuoa, kwa maelezo kuwa kuna
wanawake wamewahi kuwatesa.
Kama wewe ni kati ya watu ambao umekata tamaa na
suala la uhusiano, fahamu kuwa si wewe pekee.Kuna kundi kubwa la watu
wameshatendewa kiasi cha kufanya wasiwe na raha tena.
Mkasa wa mwanamke kukatwa mkono
Ilikuwa Agosti 7, mwaka huu, saa mbili usiku.
Ilikuwa ni siku iliyobadili historia ya maisha yake. Baada ya kuwa
katika mapenzi na mwanaume huyo kwa zaidi ya miaka 17, wakipendana na
kuitana majina yote mazuri unayoyajua yakiwamo kuambiwa ‘mpenzi wangu
nakupenda, nikinywa maji nakuona kwenye glasi’…leo mapenzi yamegeuka
shubiri.
Mwanamke huyo, Mchali Kihiyo (35), mama wa watoto
sita, aliyepoteza viungo vyake kutokana na ukatili wa kijinsia
uliofanywa na mwanaume ambaye wamekuwa na uhusiano nae (jina
limehifadhiwa).
“Uhusiano wetu ulikuwa mzuri, hata hivyo kwa sasa
naona mambo yamekuwa magumu kwangu, leo hii mimi sina mkono wa kushoto
na nimeondolewa sehemu ya viungo vyangu vya upande mmoja,”anasema
Mchali,akibubujikwa machozi kutokana na ulemavu alioupata.
Chanzo cha ulemavu
Anasema maisha yao ya uhusiano yalikuwa ya furaha
kwa kipindi chote lakini yamegeuka shubiri baada ya mwanamume wake huyo
kuonyesha dalili ya kutompenda kama awali, hali ambayo anaitafsiri kama
labda alikuwa na mwanamke mwingine.
Mchali, anasema mikasa na mateso ilianza miaka
mitatu iliyopita baada ya kuhisi kwamba mwanamume wake huyo amezaa na
mwanamke mwingine. Ubaya zaidi ulimtokea baada ya mtoto wa huyo mwanamke
mwingine, kutumbukia kwenye kisima cha maji na kisha kupoteza maisha.
“Kifo cha mtoto huyo, ndicho kilichozaa tatizo
hili la ukatili dhidi yangu na kunisababishia ulemavu, kwa kuwa huyo
mwanaume wangu na huyo mwanamke aliyezaa nae, walidai kwamba mimi ndiyo
nilimtupia majini marehemu mtoto wao ili afe,”anasema mama huyo.
Vitisho kabla ya ulemavu
Post a Comment