RIPOTI YA KUSIKITISHA TANZANIA JUU YA UBAKAJI NA ULAWITI KWA WATOTO WADOGO


 
NI sahihi kusema kuwa mwaka 2013 ni wa ubakaji, ulawiti na udhalilishaji wa watoto chini ya miaka 18 kufuatia matukio ya aina hiyo kushamiri katika jamii ambapo ripoti inatisha.
Tangu Januari hadi Septemba, mwaka huu, vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiripoti matukio hayo hadi inatisha huku vitendo hivyo vikizidi kushika kasi.
Kuna madai kwamba, wengi wanaofanya unyama huo wanaelekezwa na waganga wa kienyeji ili kujipatia utajiri, ingawa ripoti nyingi hazioneshi kama kuna ukwasi ndani yake, bali ni tabia na kushindwa kujizuia.
Watoto wengi waliokumbwa na mikasa hiyo wanakuwa na uhusiano wa karibu na watuhumiwa, kama baba mzazi, baba wa kufikia, mjomba au mtu mwingine wa jirani sana.
Mfano, mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu (jina linahifadhiwa), amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, akiwa hoi baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la John, mkazi wa jijini humo ambaye ni baba wa kufikia, kudaiwa kumbaka.
 John alidaiwa kutenda tukio hilo mwishoni mwa Agosti, mwaka huu nyumbani kwake, majira ya saa 7:00 mchana, kufuatia mama wa mtoto huyo, Christina Ruendi kutishia kuondoka zake kutokana ya kuchoshwa na manyanyaso ya mtuhumiwa huyo na chanzo kikiwa ni mtoto huyo.
Mtuhumiwa huyo alitaka mtoto huyo apelekwe kwa baba yake mzazi.
Siku ya tukio, mwanamke huyo hakuwepo nyumbani, aliporudi alimkuta mtoto wake amelala hajitambui huku sehemu ya kitanda ikiwa imetapakaa damu.
 Mama huyo alipiga kelele ambapo majirani na viongozi wa serikali wa eneo hilo, walifika na kukuta unyama alioutenda mtuhumiwa huyo bila kujali umri wa mtoto huyo na akawa ameshatoroka.
 Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamtafuta mtuhumiwa huyo huku mtoto huyo akiwa bado kwenye wodi ya watoto hospitalini hapo.
Jijini Dar es Salaam, waandishi wetu wanaripoti kuwa mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 6 (jina tunalo), amedai kulawitiwa na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Hamis ambaye ni mmiliki wa kibanda cha kuangalia video, Gongo la Mboto, Dar.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo hayo baada ya majirani kutilia shaka mwenendo wa mtoto huyo na mtuhumiwa.
Ilidaiwa kuwa baada ya kufuatilia mwenendo wao, ndipo mama aliposhtuka na kumhoji mtoto wake ambapo alikiri kuingiliwa na mwanaume huyo.
Akizungumza  kwa masikitiko, mama mkubwa wa mtoto huyo alisema alibaini kasoro kwa mwanaye huyo kwa kuwa mara nyingi alikuwa akitokwa na haja kubwa bila kujizuia, jambo ambalo lilimshtua.
“Nilimhoji akasema alikuwa akimpeleka vichakani na kumbaka halafu akipiga kelele alikuwa akimtolea kisu na kumtishia,” alisema mama mkubwa huyo.
Wazazi wa mtoto huyo waliripoti ukatili huo kwenye Kituo cha Polisi cha Gongo la Mboto, Dar na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu Hospitali ya Amana kisha wakafungua kesi yenye kumbukumbu namba GBT/RB/3018/2013 KULAWITI, mtuhumiwa anasakwa baada ya kuingia mitini.
Ukiachia mbali watoto kulawitiwa, vitendo vya kuwadhalilisha vimepamba moto nchini ambapo hivi karibuni, kikongwe wa miaka inayokadiriwa kufika sabini aitwaye Babu anakabiliwa na shitaka la kuwafungia ndani kwake wanafunzi kumi wa kike wa Shule ya Msingi Mtoni Kijichi, Temeke, Dar na kuwashika nyeti zao.
Tukio hilo lilibainika Agosti 28, mwaka huu baada ya mwanafunzi mmoja (jina tunalo) kupewa barua awapelekee wazazi wake baada ya kutoonekana shule kwa takriban miezi mitatu kumbe alikuwa anaishia nyumbani kwa kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani, mzee huyo alikiri kuwafungia ndani wanafunzi hao kwa muda waliohitajika kuwepo shuleni kwa miezi mitatu na kudai kuwa alikuwa akiwafundisha ‘twisheni’. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi hao na kufunguliwa kesi yenye kumbukumbu namba MBL/RB 8738/13 UNYANYASAJI.
Jitihada za Amani kumpata Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, zilishindikana baada ya juzi simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Amani lilizungumza na mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho nchini ambaye hakupenda jina lake liandikwe  ambapo alisema wazazi wanapaswa kumwomba sana Mungu ili watoto wao wasikumbwe na ushetani ulioenea sasa Tanzania akisema

Post a Comment

Previous Post Next Post