Serikali imesema itatumia gharama yoyote kwa ajili ya kuhifadhi
Ikolojia ya bonde la mto Mara huku ikisema itatii itifaki ya
pamoja ya makubaliano kati ya Kenya na Tanzania katika kulinda
bonde la mto Mara kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kutoka
mugumu serengeti mkoani mara,mwanahabari wetu george marato,anayotaarifa
zaidi.....Kauli hiyo imetangazwa mjini mugumu wilayani serengeti,na
waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh mizengo Peter
Pinda,katika kilele za maadhimisho ya siku ya mara ambayo yamefanyika
kwa mara ya kwanza nchini kwa kuhusisha nchi za Tanzania na
kenya lengo likiwa ni kuweka mikakati ya pamoja ya kuhifadhi bonde
la mto mara kwa sababu hiyo waziri mkuu mh mizengo pinda,amesema
lazima serikali za nchi hizi mbili wakiwemo wadau mbalimbali
kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa bonde la mto mara kutokana
na manufaa yake makubwa kwa wanyama aina ya nyumbu na hivyo kuwa
kivutio kikubwa katika sekta ya utalii kwa hifadhi za Masai Mara
nchini Kenya na hifadhi ya Taifa ya Serengeti hapa nchini ambayo ni
moja ya maajabu saba ya Dunia. Akitoa salama za kutoka nchini
Kenya, katibu mkuu wa wizara ya mazingira na maji ya nchi hiyo bw
James Teko, wakiwemo wadau wanasaidia uhifadhi wa bonde la mto
Mara, wamesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kwa kila
mdau katika kulinda na kuhidhi bonde la mto Mara. Kauli mbiu ya
maadhimisho hayo ni Mara ni mali yetu na urithi wetu tuitunze
Post a Comment