Balozi wa China akisisitiza jambo huku Balozi Kairuki akimsikiliza kwa makini.
Mkurugenzi
wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) akizungumza na
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youqing kuhusu ushirikiano kati
ya Tanzania na China.

Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana (kushoto)
akimtambulisha Balozi wa China nchini, Lu Younqing kwenye moja ya
mikutano ya chama hicho mkoani Shinyanga wiki iliyopita.

Balozi wa China nchini, Lu Younqing akihutubia kwenye moja ya
mikutano ya ccm mkoani Shinyanga wiki iliyopita.
--

Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imefuatilia taarifa kwenye
vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini, kuhusu kushiriki kwa
Mheshimiwa Lu Younqing Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini
kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
uliofanyika huko Shinyanga, mwishoni mwa juma lililopita.
Taarifa
hizo zimeambatana na picha zinazomuonyesha Mheshimiwa Lu akiwa amevaa
kofia yenye nembo ya CCM. Habari zinaeleza kuwa Balozi alikwenda
Shinyanga kuhudhuria uzinduzi wa mradi wa viwanda vya kuchambulia pamba
vinavyojengwa na mwekezaji wa Kichina anayeitwa Tahong, na viwanda hivyo
vita kuwa na uwezo wa kuchambua tani 120,000 za pamba kwa mwaka,
vitakapokamilika mwakani.
Wizara
inatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Jamhuri ya watu wa China na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vilevile inatambua kazi nzuri ambayo
Balozi Lu Younqing amekuwa akifanya toka alipowasili nchini Tanzania.
Kutokana na tukio hili, Wizara inapenda kuelekeza kwamba kitendo cha
Balozi yeyote kuhudhuria mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuvaa
sare zenye nembo ya vyama vya siasa sio sahihi na kinakiuka Kifungu cha
41(1) cha Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa
kidiplomasia.
Mkataba huo wa Vienna unazuia wawakilishi wa nchi za nje
kujihusisha na masuala ya ndani ya nchi ikiwemo siasa wanapofanya kazi
zao kwenye nchi za uwakilishi. Aidha, Sheria ya Diplomasia ya Tanzania
ya Mwaka 1986 ambayo ni zao la Mkataba wa Vienna pia hairuhusu Balozi au
mfanyakazi wa Ubalozi kujihusisha na masuala ya ndani ya nchi.
Itakumbukwa
kwamba, katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 Wizara ilikumbana na
vitendo vinavyofanana na kitendo hiki na ikachukua hatua stahiki. Na
kwa tukio hili pia Wizara imechukua hatua za kidiplomasia zinazostahili
ili kuzuia jambo hili lisitokee tena.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
18 Septemba, 2013
Dar Es Salaam.
Post a Comment