Sunderland kujenga Academy Dar


Club ya Sunderland ya Uingereza inatarajiwa kuanza ujenzi wa kituo cha michezo "Academy" katika eneo la kidongo chekundu jijini Dar es salaam kwa lengo la kuinua michezo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa biashara wa Sunderland, Gary Hotchinson, alisema ujenzi huo utaanza hivi karibuni kwa kushirikiana na kampuni ya kufua umeme "Symbion Power".

"Academy hii tunataraji kabla ya mwaka huu kuisha tayari itakuwa imeanza kujengwa na huu ni kwasababu ya ushirikiano wetu mzuri na Tanzania kwa kushirikiana na Bodi ya utalii" na aliongea kuwa Tanzania itapata mafanikio makubwa kupitia mpango huu, hasa katika sekta ya utalii.

aidha Hotchinson aliongeza kuwa licha ya kujenga kituo hicho, wanatarajia kutoa mafunzo mbalimbali ya michezo, ikiwemo ya ukocha na kupitia Club hiyo watakuwa wakizileta timu mbalimbali nchini na kuzidi kuboresha sekta ya utalii na michezo.

Nae mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dk Alloyce Nzuki, alisema wamefarijika na uhusiano huo, ambapo wanaimani kubwa kuwa sekta ya utalii itazidi kupanuka kutokana na ujio wa timu hiyo.  Habari na gazeti la Mtanzania

Post a Comment

Previous Post Next Post