Central hill Liganga iron ore
Core inspection
Drill rig on site Mchuchuma. |
Drilling Rig servicing
Exploraton shaft Mchuchuma

picha mchoro wa kiwanda chaliganga |

===== ====== ======
Tanzania kuwa miongoni wa wazalishaji wakubwa wa chuma
Afrika.
DAR ES SALAAM: Tanzania
inatarajia kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chuma barani Afrika kwa
kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka mara uzalishaji wa madini hayo utakapoanza
mwaka 2018/19 chini ya kampuni ya Tanzania China Mineral Resources Limited (TCIMRL),
ambayo ni kampuni ya ubia kati ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Shirika
la Sichuan Hongda Group (SHG) ya China.
Ripoti
ya utafiti wa TCIMRL ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kuanzishwa mgodi na
kiwanda cha chuma katika eneo la Liganga wilayani Ludewa, iliyofanywa katika
eneo la kilomita za mraba 10 pekee inabainisha kuwapo kwa tani milioni 219 za
chuma ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 70 kwa uchimbaji wa juu (open cast mining).
Eneo lililobakia lina kilomita za mraba 156 na kukadiriwa kuwa na rasilimali
kubwa zaidi.
Tanzania
itashika nafasi ya nne ikizifuatia nchi za Afrika Kusini itakayozalisha bidhaa
za chuma tani milioni 8.5 kwa mwaka, Misri tani milioni 8.0 na Libya tani
milioni 2.0 kwa mwaka. Chuma kinachozalishwa duniani ni takribani tani bilioni
1.55 kwa mwaka, mzalishaji mkubwa ikiwa ni China inayotoa tani milioni 711 kwa
mwaka ambayo ni sawa na asilimia 46 ya chuma chote kinachozalishwa duniani. Mbali
na chuma, madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni Titanium tani 175,400
kwa mwaka na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka.
Mradi
huu ni moja ya miradi miwili iliyopo katika mkataba kati ya NDC na SHG uliotiwa
saini Septemba 21, 2011 ya uanzishwaji wa mgodi wa makaa ya mawe na ujenzi wa
kituo cha kufua umeme wa megawati 600 katika eneo la Mchuchuma pamoja na ujenzi
wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 kati ya Mchumchuma na Liganga; na uanzishwaji
wa mgodi wa chuma na ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua chuma na kiwanda cha
kuzalisha bidhaa za chuma, pamoja na ujenzi wa barabara kati ya Mchuchuma na
Liganga.
Kiasi
cha Makaa ya mawe kulingana na utafiti wa TCIMRL katika eneo la kilomita za
mraba 30 ni tani milioni 370 ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka zaidi ya 100. Kkuna
eneo la ziada la kilomita za mraba 110 ambalo linakadiriwa kuwa na rasilimali
zaidi ya makaa yam awe.
Miradi
hii miwili itakayogharimu Dola za Kimarekani bilioni tatu (USD 3.0bil) inatarajiwa
kuliingizia taifa mapato ya Dola bilioni 1.7 kwa mwaka itakapoanza uzalishaji
kamili mwaka 2018/19, mapato ambayo yatatokana na uuzaji wa umeme wa megawati
600, uuzaji wa makaa ya mawe kwa nishati ya viwandani, chuma, titanium,
vanadium na itatoa ajira ya moja kwa moja watanzania 6,000 na 35,000 kwa zisizo
za moja kwa moja.
Miradi
hii hivi sasa ipo katika awamu ya kwanza ambayo ilikuwa inahusisha utafiti na
maandalizi kabla ya Mei mwakani kuingia katika awamu ya ujenzi wa migodi na
viwanda katika maeneo ya Mchuchuma na Liganga.
Mradi
huu wa ubia na mwekezaji wa kimataifa unakwenda sambamba na mradi mwingine
katika eneo hilo la Ludewa uliotiwa saini Septemba 2, 2009 na kampuni ya wazawa
ya M.M. Steel Resources Public Limited Company (MMSR PLC). Mradi huu unalenga
kuzalisha chuma ghafi kwa kutumia chuma cha Liganga Matitu na makaa ya mawe ya Katewaka. Kampuni ya ubia
iliyoanzishwa ni Maganga Matitu Resource Development Limited (MMRDL). Uwekezaji
utakuwa ni dola za Kimarekani milioni 150 na unatazamiwa kuingiza mapato ya
dola milioni 183.3 kwa mwaka. Chuma ghafi hiki kitatumika kuwa malighafi kwa
viwanda vingine vilivyo ndani na nje ya
nchi, hivyo kuwezesha uzalishaji wa chuma imara kulikoni hiki cha sasa
kitokanacho na scrap ambacho ni hafifu. Lakini pia hujuma kwa miundombinu yetu
kwa ajili ya scrap utakoma.
Imetolewa
na: Abel Ngapemba
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika
angapemba@ndc.go.tz,
022 211 1490 0784 273 588/0715
18 Septemba 2013
Post a Comment