Adubo Mustafa Omer Enzi ya uhai wake
Baada ya uchunguzi wa zaidi ya
wiki tatu,Ubalozi wa Tanzania Washington DC umethibitisha kuwa Marehemu
Adubo M. Omer hakuwa Raia wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania bali
alikuwa Raia wa Sudan.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa
Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Dar Es Salaam ilielezwa kuwa,hakuna
kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa, Marehemu Adubo aliwahi kupewa
Uraia wala Pasipoti ya Tanzania.
Aidha,kwa mujibu wa taarifa
zilizopatikana na kuthibitishwa kutoka kwenye taasisi mbali mbali za
Kiserikali zilizopo mjini Dallas Texas, Marehemu Adubo M Omer alizaliwa
tarehe 25.04.1956 katika sehemu iitwayo Maridi Abang, iliyopo Sudani ya
Kusini.
Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa
marehemu Adubo, alikuwa amepewa hati ya kudumu ya ukaazi Nchini Marekani
(Permanent Resident card) ambayo ilikuwa inamaliza muda wake tarehe
8.03.2014.
Ubalozi ulipotaka kujua, ilikuwaje
hadi ofisi ya 'Medical Examiner' ambayo inafanya uchunguzi wa sababu za
kifo cha Marehemu Adubo imtambulishe ubalozini marehemu huyo kama Raia
wa Tanzania? Msemaji wa ofisi hiyo alieleza kuwa, hii ni kwa mujibu wa
maelezo ambayo marehemu mwenyewe aliyatoa kwenye kituo cha Police cha
Dallas, alikokuwa amekamatwa na kuwekwa ndani kwa siku chache kisha
akaachiwa kabla ya kifo chake.
Inaelekea Marehemu Adubo hakutaka
Uraia wake ujulikane kwa sababu ambazo hazikuweza kueleweka. Suala hili,
lilileta utata na hisia ambazo zimeuletea Ubalozi usumbufu ambao
haukuwa na ulazima wowote.
Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania
washington DC, inapenda kuwashukuru Watanzania wote waliopo Ndani na Nje
ya Nchi waliosaidia katika jitihada za kupatikana kwa taarifa sahihi za
mtu huyu. vile vile Ubalozi unazishukuru taasisi zote za hapa Marekani
ambazo kwa namna moja au nyingine zimetoa ushirikiano wenye tija
uluotuwezesha kulitatua suala hili.
Shukurani za pekee, ziwaendee
blogs za vijimambo na swahili villa, bila kuwasahau uongozi wa jumuia ya
Watanzania waishio Dallas Texas, Bw Franklin Maji, Mchungaji Absalom na
Bi aysha Burnett.
IMETOLEWA NA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA
WASHINGTON DC.
Post a Comment