• Wateja wanaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za benki
kwenda kwenye akaunti ya Airtel money masaa 24 siku 7 za wiki.
• Ni njia salama, rahisi ya kupata pesa kupitia kutoka Airtel
Airtel
Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel money imeanzisha ushirikiano na
benki mbalimbali nchini na kuwawezesha wateja wake kuhamisha pesa kutoka
kwenye benki akaunti zao na kuziweka kwenye akaunti ya Airtel
money. Benki ambazo zimeingia katika ushirikiano huo na Airtel ni pamoja
na Tanzania Postal Bank, Bank of Africa, Kenya Commercial Bank,
Barclays Bank, Akiba Commercial Bank, Exim Bank, Amana Bank,
Mkombozi Commercial Bank na Standard Chartered bank.
Akiongea
juu ya ushirikiano huo Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi. Beatrice
Singano Mallya (pichani) alisema” kuanzishwa kwa mpango huu wa
huduma ya Airtel money na za kibenki kutawawezesha wateja Airtel kutoa
pesa kwenye akaunti zao za benki na kuziweka kwenye simu zao yani
akaunti ya Airtel money kirahisi bila kutembelea ofisi za benki. Huduma
ya Airtel Money ni suluhisho la huduma za kifedha ikiwa na zaidi ya mawakala
20,000 , kupitia mtandao wetu mpana ulioeneea nchi nzima tunauhakika wa
kuwafikia watu wengi zaidi hasa wa maeneo ya vijijini”
Tunaamini
ushirikiano na benki zingine kutaendelea kuwaletea wateja wa huduma ya
Airtel money ufanisi na urahisi wa upatikanaji wa fedha kutoka kwenye
benki zao wakati wote mahali popote nchi nzima.”
Mallya
aliendelea kusema Airtel imedhamiria kutoa huduma za kiubunifu kwa
watanzania kwani tunatambua tecknologia ya simu inazidi kukua
na kuunganisha watu na kubadili maisha ya jamii. Huduma ya Airtel money.
inatoa
mwanya kwa makampuni, watoaji huduma za kitechnologia inawezesha huduma
za malipo na kukuza huduma za kifedha nchini. Airtel imejipanga kutoa
huduma za kifedha na kuiwezesha kuwa ya mafanikio aliongeza Mallya.
Akiongea
kuhusu ushirikiano meneja huduma wa Airtel Money Bw ,
Asupya Nalingingwa Alisema” tunafuraha kuingia kwenye makubaliano haya
ya ushirikiano wa kutoa huduma za kifedha na benki hizi tofauti ambapo kwetu
ni nafasi nzuri ya kuendelea kuboresha huduma za kifedha nchini na
kuwafikia wateja wa benk hizi na wateja wa Airtel wasio na huduma ya
benki hizo maeneo ya karibu.
Ili
kupata orodha ya huduma za benki husika mteja anatakiwa kupiga namba
zifuatazo na kufuata maelezo Tanzania Postal Bank –*150*21#, Bank of
Africa –*150*13#, Kenya Commercial Bank –*150*22#, Barclays
Bank
–*150*20#, Akiba Commercial Bank –*150*10#, Exim Bank –*150*11#, Amana
Bank –*150*12#, Mkombozi Commercial Bank –*150*06# , Standard Chartered
Bank – *150*65#
Huduma
ya Airtel money inawawezesha wateja kulipia bili zao, kutuma na kupokea
pesa na kufanya miamala mbalimbali, huduma hii inapatikana kwa wateja
wa malipo ya awali na ya kabla , kujiunga na huduma hii ni bure kwa
kupita maduka ya Airtel na mawakala nchi nzima. Mpaka sasa
Airtel Money inamawakala zaidi ya 20,000 Wanaotoa huduma za kifedha
kwa wateja nchini. Airtel inatoa huduma ya Airtel money kwa msharika
na watu binafsi kama njia mbadala ya malipo.
Airtel
pia kupitia Airtel Money kwa sasa imezindua promosheni mpya ya Hakatwi
mtu hapa inayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bila
makato yoyote popote pale nchini.
Post a Comment