MSHINDI
wa taji la Redd’s Miss Tanzania mwaka huu anatarajiwa kuondoka na gari dogo
lenye thamani ya Sh milioni 15, huku akipewa kitita taslimu cha fedha cha Sh
milioni 8.
Shindano
hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 21, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani
City, huku kukiwa na burudani za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu wa ndani
pamoja na mwingine kutoka nje.
Akitangaza
zawadi hizo jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original,
Victoria Kimaro alisema, wameamua kutangaza mapema zawadi hizo, ili kuleta
morali kwa washiriki wote wa shindano hilo.
“Tunaamini
shindano la mwaka huu litakuwa na ushindani mkubwa zaidi na zawadi hizi
zitakidhi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya warembo,” alisema Victoria. Shindano
hilo litashirikisha warembo 30 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Mbali
na mshindi kutwaa zawadi hizo, mshindi wa pili atapata Sh milioni 6.2, mshindi
wa tatu Sh milioni , mshindi wa nne Sh milioni 3, mshindi wa tano Sh milioni 2,
mshindi wa sita hadi 15 atapata Sh milioni 1.2 na waliobaki watapata Sh 700,000
kila mmoja.
“Thamani
ya fedha taslimu itakuwa ni kiasi cha Sh milioni 46.1 na zawadi zote hizi
watakabidhiwa warembo wa Redd’s Miss Tanzania siku inayofuata baada ya
kufanyika kwa fainali hizo,” alisema Victoria.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio
waandaaji aliwashukuru wadhamini na kusema wamefanya kazi kubwa zaidi
katika kuyakuza mashindano hayo.
“Kwa
mara nyingine tena tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wetu
wakuu Redd’s Original na wadhamini wenza ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa
sana kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa zuri zaidi,” alisema Lundenga.
Taji
la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred aliyelitwaa
taji hilo mwaka jana na kukabidhiwa gari aina ya Noah pamoja na kitita cha Sh
milioni 8.
Nafasi
ya pili katika shindano hilo alikuwa Eugene Fabian kutoka Kanda ya Ziwa, Edda
Sylvester aliyekuwa Miss Temeke akishika nafasi ya tatu, ya nne ikienda kwa
mrembo kutoka Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya tano ikienda Happyness
Daniel kutoka Kanda ya Ziwa.
Shindano
la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
kinywaji chake cha Redd’s Original, huku wadhamini wenza wakiwa Zanzi, Giraffe
Hotel, Star TV, Nipashe, Uchumi Supermarket, Marie Stopes na Clouds FM.
Post a Comment