Benki ya NMB jana iliendesha droo yake ya kwanza katika
promosheni ya Ki-COLLEGE Plus na NMB iliyochezeshwa katika Makao Makuu
ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Jumla yawashindi 20 wamepata bahati
ya kujishindia simu za mkononi aina ya ‘Samsung Galaxy Pocket Plus 3g’
na washindi wengine 100 kujishindia fulana za NMB.
Katika promosheni hii inayoendelea hadi tarehe 15 Januari, 2014, ,
wanafunzi watakaoendelea kufungua NMB Student Account wataendelea
kufurahia huduma za NMB Student Account kama: Kufungua akaunti kwa Sh.
10,000 tu itakayokuwezesha kupata kadi ya ATM ya NMB), kujiunga na
huduma ya NMB mobile bure, kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo
fedha kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1, 000,000 kwenye
NMB ATM kwa siku na kupata huduma kupitia matawi zaidi ya 150 na NMB ATM
zaidi ya 500 nchi nzima.
Ili uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishia Zawadi
kwenye promosheni ya Ki-COLLEGE Plus na NMB, mwanafunzi wa elimu ya juu
anatakiwa kufungua NMB Student Account, kuweka amana katika akaunti ya
NMB Student Account, kutumia au kujiunga na NMB mobile. Ikiwa hujatumia
akaunti yako kwa muda mrefu, tembelea tawi la NMB lililo karibu nawe ili
uweze kupata huduma itakayokuwezesha kuanza kutumia akaunti yako, ili
nawe ushiriki katika promosheni hii ya Ki-COLLEGE plus
Post a Comment