Baada Ya Ujerumani Ni Switzerland, Kwa Ajili Ya Kupiga Show - Ally Kiba

kiba1
Msanii mahiri aliyesaidia sanaa ya bongo fleva kukuwa hapa nchini Ally Kiba, kwa sasa imeripotiwa  yupo nchini Ujerumani ambapo msanii huyu alikwenda nchini humo kwa ajili ya kupiga shoo siku ya tarehe saba, kwa  ajili ya kuwaburudisha wapenzi wa muziki wake walioko nchini humo katika jiji la Frankfurt Ujerumani.
kiba 2
Na sasa msanii huyu antarajia kuelekea nchini Uswiss kwa ajili ya kwenda kuwaburudisha wapenzi wengine wa muziki wake walioko katika jiji la Zurich. Ally Kiba anatarajiwa kufanya shoo hiyo Zurich tarehe 14.
kiba3
Ila kwa sasa msanii huyu yupo bado nchini Ujerumani kwa mapumziko ya muda kabla ajaondoka nchini humo kwenda Switzerland… Na pia yasemekana msanii huyu anatarajia kuhudhuria mechi ya Bayern Munich dhidi Manchester City hapo baadae.

Post a Comment

Previous Post Next Post