Msanii wa muziki wakizazi kipya nchini Tanzania Baby Madaha katika poz
Hatua ya Baby Madaha kuwa msanii wa kwanza mwanamke nchini Tanzania,
kujitokeza hadharani kumchambua msanii huyo mkubwa na mwenye heshma
kubwa ndani na nje ya nchi, imevuta hisia za wadau wa muziki nchini huku
akimwagiwa sifa kemkem kwa kujitokeza na kufuangua ufahamu wa wasichana
kutokana na imani kwamba Diamond ni mchawi anayetumia nyota za wanawake
kujipatia umaarufu.
Baby madaha ambaye anatarajia kuzindua Single nne pamoja na muvi yake
kali zilizotengenezwa nje ya nchi, amesema kwamba kinachomkera zaidi ni
kitendo cha Diamond kudhalilisha wasicha wenzake kimapenzi, kila kukicha
kutoka na uwezo wake wa kifedha huku akitangaza wazi kwamba anafanya
mapenzi bila kutumia kondom kwa madai kwamba anatafuta mtoto.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania,Baby Madaha akiwa
katika poz,Akizungumza na Habarimpya.com Baby Madaha alisema
kwamba,uzinduzi wa kazi yake itafanyika katika Hotel ya Golden Tulip
ambapo atatumia uzinduzi huo kumwonyesha Diamond kwamba wanawake si
chombo cha starehe kama anavyo fikiria, huku akimwonyesha kwamba yeye ni
Queen Of Swagg (QOS), na kwamba staili hiyo itafunika staili ya ngololo
ya single moja iliyobeba uchafu wa ngono na uchawi ndani ya Album yake
iliyozinduliwa katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
"Tarehe 22 Jumapili Disemba mwaka huu pale Golden Tulip nitamuonyesha
Diamond,kuwa Queen of Swagg ni nani,ambapo yeye alizindua Single moja ya
ngololo pale Serena mimi ninazindua single 4 moja ikiwa ni Soundtrack
na Move yangu mpya ya the Galbladder, iliyonigarimu mamilioni
kuitengeneza nje ya nchi,huku show nzima ikidhaminiwa na Heinekein ambao
pia ndiyo wadhamini wa lebo ya Candy& candy ya jijini Nairobi, huku
mgeni rasmi akitarajiwa kuwa kiongozi mzito kutoka Ikulu ya Rais
Kikwete pale Magogoni jijini Dar es Salaam"alisema Baby Madaha.
Kuhusu kauli yake kwamba Diamond ni mchawi alisema kwamba, "ingawa kuna
maneno mengi kwamba Diamond ni mchawi na kwamba anaweza kuniroga, mimi
hilo halinitishi kwa sababu yeye anashindana na wanawake badala ya
kushindana na wanaume wenzake, katika maendeleo ila ukweli ni kwamba
mimi si shindani na wanwake kwa sababu ni marafiki zangu, ila
ninashindana na wanaume katika suala la maendeleo na siamini katika
uchawi na akiona kwamba anaweza kuniroga kama ambavyo watu wake
wananitangazia ajaribu,kwani mimi ninazungukwa na nguvu za Mungu na si
Nguvu na Mganga wa kienyeji".
Baby Madaha alisema kwamba baada ya kumwangusha nyota huyo wa muziki
nchini na kumfanya afikirie kumroga katika uzinduzi huo ataanza kufanya
ziara nchini nzima kuitangaza Queen of Swagg itakayozidi kuipoteza
ngololo ya Diamond katika ramani ya muziki ndani na nje ya nchi, kabla
ya kuendelea na show kali sehemu mbalimbali Dunaini kama ilivyo pangwa
na wanadhamini wkake wakuu Heinekein.
Post a Comment