
Mandela na aliyekuwa mkewe Winnie Mandikizela
Maelfu ya watu wanaendelea
kuwasili katika uwanja mkubwa wa FNB mjini Johanessburg kwa ajili ya
misa ya wafu ya hayati Nelson Mandela,
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia
watakaohudhuria misa hiyo.Misa hiyo itafanyika katika uwanja wenye viti vya watu 95,000 ambako Nelson Mandela alionekana mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya viowanja ili kuzuia watu kujaa pomoni katika uwanja huo.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.
Post a Comment