Masoud
Kipanya, Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus, akizungumza na wananchi
waliofika kushuhudia uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013
Kingolwira Morogoro , pia kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya
Mvomero Mh. Anthony Mtaka kufanya uzinduzi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza na wakazi wa eneo
la Kingolwira pamoja na wageni na kutoa tamko rasmi la kuzindua
shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013.
Mshindi
wa Shindano la Maisha Plus, Bernick Kimiro, akizungumza na wageni
waalikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa
kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano
la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimeanza
kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za
kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.
Bwana Bonda ambaye ni mmoja wa wakurugenzi Maisha Plus.
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula 2013 Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akifanya uzinduzi wa aina yake
wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012/13 kwa kufukua fomu ambazo
zilikuwa zimefukiwa ikiwa ni kielelezo cha kilimo kwanza.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akimkabidhi Fomu ya
kwanza ya ushiriki kwa Bi. Nuru Saidi Mbonga kutoka Dakawa ikiwa ni fomu
ya Mama shujaa wa Chakula 2013
Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya
Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani
Mmoja ya Vijana wakiume nae akiwa anakabidhiwa fomu ya ushiriki na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka
Wakiwa wanasoma fomu na kujiandaa kuzijaza
Burudani za Ngoma zikiendelea
Burudani za aina yake zikiendelea
Wazee kutoka eneo la Kingolwira wakiwa wamekuja kushuhudia uzinduzi huo
Wadau kutoka Sehemu mbalimbali wakiwa wamekuja shuhudia uzinduzi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Ali Masoud 'Kipanya' akifunga sherehe fupi za uzinduzi wa Maisha Plus 2013
Post a Comment