Ni habari za kusikitisha zilizompata mkongwe huyu wa miondoko ya R & B, Mary J. Blige ambaye amejikuta kwenye heka heka na hofu kubwa baada ya baba yake mzazi, Thomas Blige,63, kukimbizwa hospitali huko Michigan, Marekani kutokana na kuchomwa kisu (Multiple stabs) jana Alhamisi asubuhi, maeneo ya shingoni baada ya kutokea mtafaruku kati yake na “Ex Girlfriend” wake baada ya ugomvi kati yao, gazeti la kila siku toka Battle Creek, Michigan limeripoti..
Polisi walimkuta baba wa mwanamuziki huyo akiwa na majeraha matatu kutokana na kuchomwa na kisu, ambacho nacho kilikutwa kwenye eneo la tukio kama silaha iliyotumika na ndipo alipowahishwa hospitali na baada ya hapo kufanyiwa operesheni ndogo ili kufunga vidonda vyake. Hali yake bado haijaimarika mpaka asubuhi ya leo.
Mwanamke huyo alikamatwa na polisi na kuwekwa chini ya ulinzi wa mahabusu ya Calhoun County ambapo atasubiri kupandishwa kizimbani leo Ijumaa.
Source: BattleCreekEnquirer.com

Post a Comment