Wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari ya Mustapha Sabodo iliyoko katika
kijiji cha Msijute Halmashauri ya Mtwara Vijijini, mkoani Mtwara
wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari wakati wakikimbia
mchakamchaka jana alfajiri.
Wanafunzi hao walikufa baada ya kugongwa na gari aina ya Mercedes-benz namba T174 AED jirani na eneo la shule.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea alfajiri saa 11:40 katika maeneo ya shule hiyo barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi na kwamba gari hilo lililokuwa katika mwendo wa kasi, lilikuwa linaendeshwa na Baraka Mgengwe (50) wakati likitokea Mtwara kwenda Lindi.
Kamanda Stephen hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na mazingira ya ajali hiyo, mbali ya kusema kuwa wanafunzi hao walipatwa na mkasa huo wakati wakigeuka kurejea shuleni.
Alisema kuwa wanafunzi 21 walijeruhiwa huku wengine 26 waliopata mshtuko, walitibiwa kisha kuruhusiwa.

Post a Comment