Mwenyekiti wa
CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini
Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya
Mapinduzi.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa
mjini Zanzibar kuhusu yale yaliojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashuri Kuu ya CCM Taifa na pia kutangaza uteuzi wa Ndugu Mahmoud
Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa nafasi ya
uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabit Kombo mara
baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumteua kuwa mgombea
wa nafasi uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM.
Picha na Adam H. Mzee



Post a Comment