
“KAMA
nisingekuwa staa Chelsea, ningalicheza mirindimo ya samba Brazil.” Hiyo
ni kauli ya Willian Borges da Silva maarufu kama Willian, nyota wa soka
wa Brazil anayekipiga Chelsea.

Willian
anasema soka ilikuwa kwenye damu kiasi cha kutotilia umuhimu wa shule,
kwamba hata kazi alizopewa shuleni kwa ajili ya kuzifanya nyumbani
akimpa mama yake amfanyie.
Anasema
alikuwa ‘bize’ zaidi katika kucheza soka kama ambavyo wanavyofanya
watoto wengi nchini Brazil, kwamba kila wakati alikuwa na mpira mguuni.
Willian
anasema kuwa alitazama fainali za Kombe la Dunia 1998 akiwa na umri wa
miaka tisa, na alitaka kuwa Ronaldo de Lima au Zidane ambaye alimvutia
mno kwenye fainali hizo zilizofanyika Ufaransa.
“Kama
nisingalifanikiwa kama mwanasoka, sina hakika ni nini ningefanya. Labda
ningalikuwa napiga muziki Brazil,” alisema staa huyo anayependa kupiga
ala mbalimbali za muziki kama Percussion, drum na pandeiro.
Willian
mwenye umri wa miaka 25, mwenye uwezo wa kushambulia kutokea kulia,
sambamba na kusaidia ulinzi na kutengeneza nafasi, amefanikiwa kuteka
akili ya Jose Mourinho kiasi cha kumwamini dimbani na kumwacha benchi
Juan Mata
Post a Comment