
Hollande na Vallerie
Mama wa taifa nchini Ufaransa
Valerie Trierweiler amelazwa hospitalini baada ya vyombo vya habari
nchini humo kudai kuwa Rais Francois Hollande ana mchumba wa kando.
Rais Hollande anaishi na Valerie ingawa hawajaoana rasmi.Bwana Hollande hakukanusha madai hayo ingawa aliteta vikali kuhusu vyombo vya habari kuingilia maisha yake binafsi.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Conservative, Jean-Francois Cope amesema kuwa taarifa hiyo imeharibu sifa ya Ufaransa kimataifa.

Gayet mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais Hollande
Hii leo Rais Hollande alitarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa nchi hiyo ingawa mambo yanaonekana yatabadilika kutokana na taarifa hizi kuhusu kashfa ya mapenzi inayomwandama Hollande.
Trierweiler na Hollande walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1988 akiwa mwandishi wa habari wakati huo nayeHollande akiwa mbunge wa chama cha kisosholisti.
Kura za maoni zinaonyesha ushawishi wa Hollande kudidimia na kwamba ni 25% pekee ya watu nchini humo wana Imani naye.
- bbc swahili
Post a Comment