
Wanaharakati wakipinga ubakaji nchini Morocco
Bunge nchini Morocco, limepiga
kura kwa kauli moja kufanyia marekebisha sheria iliyoruhusu wanaume
waliowabaka wasichana kutofunguliwa mashtaka, ikiwa watawaoa waathiriwa
wao.
Kura hiyo imepigwa takriban miaka miwili baada
ya msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na sita, Amina al-Filali,
kujiua baada ya kulazimishwa kuolewa na mtu aliyembaka.
Wazazi wa msichana huyo na jaji mmoja, waliruhusu ndoa hiyo ili kulinda hadhi na heshima ya familia hiyo.
Kesi hiyo iliwashangaza watu wengi nchini
Morocco mbali na kusababisha maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi
hiyo Rabat, na miji mingine mikuu.
Wanaharakati wa kutetea haki za kina mama wameafiki mabadiliko kwenye kifungo hicho cha sheria.
Chini ya katiba ya nchi hiyo mtu aweza kuoa au kuolewa baada ya umri wa miaka kumi na minane
Post a Comment