VIDEO YA ‘KULA GAMBE’ BY SHILA KUACHIWA WIKI IJAYO


VIDEO YA ‘KULA GAMBE’ BY SHILA KUACHIWA WIKI IJAYO
Ile ngoma ‘KUla gambe’ kutoka kwa cute one Shillavirgy au Shillah ambayo imeingia mtandaoni tu kwa hapa Tzee ikisubiri kichupa chake kikamilike ili iingie media rasmi huku pande za Uganda ikiwa tayari imeanza kupata airtime ya kutosha, kichupa chake kipo mbioni kuachiwa.
Akiongea na Baabkubwa meneja wa msanii huyo amesema kuwa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni hatua za mwisho tu za mambo flani ya kisheria kabla ya kuiachia hewani rasmi.
“Video imekamilika ambayo imefanywa na ‘Badi Film’ ya Uganda wale jamaa waliofanya video ya Valuvalu na nyingine nyingi tu za wasanii wote wakubwa ya Uganda, lakini kwa sasa kuna mambo ya kisheria yahusuyo ofisi zao kidogo ndio tunamalizia kabla ya kuiachia rasmi pande za Bongo. Ni video kali na watu waisubiri wenyewe wataongea.” Alisema meneja huyo.
Ngoma hiyo ambayo ipo kwenye mahadhi ya Dancehall na Reggae Maffin inafanya vizuri pande za Uganda mara baada ya kuachiwa rasmi kwenye radio waves za huko.
“Tunamshukuru Mungu coz hii ngoma inafanya poa sana Uganda kwa kuwa tulishairelease officially but home tunaiachia rasmi na kichupa chake. Ila hata video media za Uganda zimeomba sana tuwaachi so kesho video tunairelease rasmi huku then tunarudi Dar na ndani ya wiki hiyo hiyo tutaiachia rasmi kwa media zote yaani video na audio ya ‘Kula Gambe’. Tunaomba sapoti sana kwa Watanzania wenzetu.” – Aliongea meneja huyo akiwa pande za Uganda alipokwenda kuchukua hiyo video.
Isikilize hapa audio ya ngoma hiyo
 

Post a Comment

Previous Post Next Post