Ade: A Love Story - Ni filamu ya Kenya inayoongozwa na Madonna

Director-MadonnaMsanii wa muziki kutoka Marekani, Madonna anatarajia kuhusika katika kazi ya kuongoza filamu itakayofanyika nchini, Ade: A Love Story.

Director Madonna
Filamu hiyo ya mapenzi ni juu ya binti wa kimarekani wa miaka 19 ambaye alifika katika pwani ya Kenya na kuangukia katika penzi la kijana wa Kiswahili aitwaye anayeitwa Ade ambaye naye anampa jina ‘Farida’ na kuanzisha mahusiano ambayo yanakumbana na vikwazo mbalimbali. Kisa chake kinatokana na kitabu cha hadithi cha mwandishi Rebecca Walker. Filamu hii inaongeza rekodi ya filamu ambazo Madonna amekwishashiriki kuongoza, ikiwemo ile ya W.E. na Wallis Simpson and Filth and Wisdom.

Post a Comment

Previous Post Next Post