Kaimu mkurugenzi wa biashara
na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania, Juma Boma (wa pili
kulia) akipanda ndege mpya aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege Julius
Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege wakimataifa
wa Songwe. Shirika hilo limeanza safari zake kwenda Mbeya ambapo
itaruka mara nne kwa wiki.
Kaimu
mkurugenzi wa biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania
(ATCL) Juma Boma akipokea maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege
hiyo, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200
iliyotumika kuzindua
safari za kati ya Dar es Salaam na Songwe. Nyuma yake ni kaimu
mkurugenzi wa ufundi, Patrick Itule. Shirika hilo litakuwa linaruka mara
nne kwa wiki kwenda Mbeya.
Kaimu mkurugenzi wa biashara
na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma,
akibadilishana mawazo na Kaimu mkurugenzi wa ufundi wa shirika hilo,
Patrick Itule, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya
CRJ-200 inayotumika katika uzinduzi wa safiri kati ya Dar es S alaam na
Mbeya. Shirika hilo litakuwa likifanya safari zake mara nne kwa wiki
kwenda Mbeya, safari ya lisaa limoja tu.
Meneja
wa Kanda ya Mbeya wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL), Shabani
Mtambalike (kulia), akimkaribisha Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko
wa ATCL, Juma Boma (wa pili kulia) na kaimu mkurugenzi wa ufundi
Patrick Itule muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa
Songwe Jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya
CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.
Kaimu mkurugenzi wa biashara
na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma (wa pili
kulia, Kaimu mkurugenzi wa ufundi Patrick Itule (wa tatu kulia) na
Meneja wa Kanda ya Mbeya wa shirika hilo Shabani Mtambalike (kulia)
wakishangilia, pamoja na wageni wengine, kuwasili kwa ndege ya ATC
katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe jumatatu mchana. Shirika hilo lilitumia ndege yake mpya aina ya CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki.
Kaimu mkurugenzi wa biashara
na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania Juma Boma akikata keki
kama ishara ya kuzindua safari za ndege ya ATCL kati ya Dar Es Salaam na
Mbeya, hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Songwe siku ya
Jumatatu mchana. Shirika hilo la ndege lilitumia ndegeyake mpya aina ya
CRJ-200 kuzindua safari zake ambapo itasafiri mara nne kwa wiki
Abiria wakiwa ndani ya ndege mpya ya Air Tanzania aina ya CRJ-200 muda mfipi kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Songwe wakitokea Dar es Salaam.
Abiria
wakipanda ndege ya Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya
CRJ-200 katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe wakielekea Dar es
Salaa. Safari hizi zitafanyika mara nne ndani ya wiki.
======== ======== =========
ATCL yaanza safari za kwenda Mbeya
Shirika
la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Jumatatu hii lilizindua safari zake za
kwenda Mbeya kupitia uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Songwe
likitumia ndege yake mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 50 ya Canada aina
ya CRJ – 200.
Safari
hiyo inayochukua kadri ya saa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya
itakayofanyika siku nne kwa wiki; Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na
Jumapili, ililakiwa na abiria na wafanyabiashara wanaosafiria kutoka
Mbeya kwenda katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kihistoria uliofanyika katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Songwe, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara/Masoko wa shirika hilo
Bw. Juma Boma alisema Air Tanzania imerudi kwa kishindo katika mji ambao ni kitovu cha biashara kwa mikoa ya nyanda
za juu kusini na inayotumika kama njia ya kuiunganisha Tanzania na nchi
za Kusini mwa Afrika, ili kupunguza adha
ya usafirina kuiunganisha sehemu ya Kusini mwa Tanzania na mikoa
mingine.
“Safari
ya Air Tanzania kwenda Mbeya iliyosubiriwa kwa muda mrefu imeanza rasmi
leo hii. Kwa kutumia ndege yetu mpya, tunatoa usafiri wa haraka na
salama, tukiiunganisha Mbeya na mikoa mingine. Kwa saa moja tu, abiria
wetu wanauhakika wa kutua uwanja wa ndege wa Songwe kutokea Dar es
Salaam.
“Tumezingatia
masuala yote ya kiuchumi ili kupanga nauli tuliyoanza nayo ambayo ni
kiasi cha shilingi 150,000 kwa tiketi ya kwenda na shilingi 260,000 kwa
tiketi ya kwenda na kurudi,” alisema,” Bw. Boma.
Alisema
uzinduzi wa njia ya Mbeya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati
madhubuti wa upanuzi wa shirika, ambao umelenga katika kuzirejesha
safari zote za ndani na za kimataifa na kufungua njia nyingine mpya.
Boma
alisema kuwa kutokana na mkakati wao ujulikanao kama go-green
utalipelekea shirika hilo la ndege la taifa kuongeza toleo jipya ya
ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 78 mwishoni mwa mwezi
Mei mwaka huu, shirika hilo litaongeza idadi ya safari zake katika njia
zake kuu na kuongeza safari za kimataifa.
“Kupitia
upanuzi wa safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku
kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondokea Dar ukiwa ni
saa 11 jioni na kutokea Mwanza ni saa moja usiku. Tutakuwa tukienda
mwanza mara nne kwa wiki.
Tutakuwa
pia tukisafiri kwenda Moroni nchini Comoro katika siku za Jumatatu,
Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Vile vile tunatarajia kufungua njia ya
Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.
Alibainisha
kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria
wanaoshindwa kutokea wakati wa safari na wale wanaobadilisha ratiba ya
safari zao, na kusema kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama
za ziada endapo watakumbana na dharura mbali mbali kabla ya safari.
Mmoja
kati ya abiria aliyesafiria katika ndege hiyo kwenda Mbeya, Deogratius
Nyanshile aliipongeza Air Tanzania kwa maamuzi yake na kutoa wito kwa
watanzania kuliunga mkono shirika kwa kusafiria na Air Tanzania.
“Nawaasa
wakazi wa mkoa wa Mbeya na kanda ya kusini kwa ujumla, kuitumia fursa
hii kikamilifu iliyotolewa na shirika la Ndege la Air Tanzania,” alisema
Nyanshile. Ndege hiyo ya taifa,
ambayo ilisimamisha huduma zake katika mkoa huo kwa sababu ya ubovu wa
uwanja wa ndege wa zamani wa Mbeya, imerejesha safari hizo baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.
Ikitumia ndege yake aina ya Bombardier Dash-8, ATCL kwa
sasa shirika hilo linasafiri katika zaidi ya sehemu naneTanzania ikiwa
ni pamoja na Mtwara, Mwanza,
Tabora,Kigoma, Dar es Salaam, Bujumbura, Mbeya na kwendaMoroni nchini
Comoro.
Post a Comment