Davido awaomba radhi mashabiki wa New York baada ya show yake kukatishwa na polisi kwa kujaza kupita kiasi - Video:

Davido (1)
.


Ijumaa iliyopita Star wa Nigeria Davido alikuwa anatarajiwa kufanya show New York, Marekani show ambayo imeacha historia ya kupata watu nyomi kiasi cha kusababisha hadi polisi wa New York kuingilia kati na kuifunga kwa sababu za kiusalama kutokana na wingi wa watu.
Show ya New York ndio ilikuwa ya kwanza katika tour yake ya Marekani na Canada, na hiki ndicho alichokiandika Instagram baada ya show hiyo kuzuiwa na polisi.
“Damn! My NY was too packed, police shut it down! The love and support that came out was overwhelming!!! I will be back! Really Sad!”
Tazama video (hapo juu) ya jinsi show hiyo ya New York ilivyojaa watu pamoja na Davido akiomba radhi mashabiki wake wa New York kwa kile kilichotokea.

Post a Comment

Previous Post Next Post