Exclusive: Mzozo kuhusu M-Rap na B'Hitz undani uko hapa..

 
Inawezekana umesikia mengi kuhusu mzozo na tofauti iliyopo hivi sasa kati ya rapper aliyekuwa chini ya usimamizi wa B’Hitz, MRap Lion na producer wa studio hizo, Pancho Latino lakini mzizi wa mzozo huo ukawa unakuchanganya.
Kwenye kila malumbano au kutokuelewana lazima kuna sababu za mbali na sababu za karibu (long term causes na short term causes), tovuti ya Times Fm imeamua kuzama ndani kuangalia nini hasa chanzo cha ugomvi huo ambao uliibua mapya juzi baada ya B’Hitz kuachia wimbo wa MRap ‘Nishike’, siku chache baada ya MRap kuachia wimbo wake aliomshirikisha Jux ‘Usiende Mbali’. Hapo ndipo tulipoanzia.
MRap aliiambia Bongo5 kuwa hautambui wimbo huo japo yeye ndiye aliyeuimba na sababu kubwa ikiwa umetoka bila ridhaa yake.

Hata hivyo, uongozi wa B’Hitz haujasema chochote kuhusu kuondoka kwa rapper huyo huku ukiachia nyimbo mbili ‘Nishike’ na Only You aliomshirikisha Jux.

Baada ya kupata tips kadhaa na chanzo kimoja, tovuti ya Times Fm imemtafuta mtu ambaye alipewa kazi ya kushughulikia promotion za kazi za B’Hits ambaye anafahamika kwa kazi hizo hapa mjini, jamaa anaitwa Shabaha na kupiga nae story na kisha kumtafuta MRap ili kubalance yale yaliyosemwa.

Kwa mujibu wa Shabaha, yeye alipewa tenda ya kuhakikisha anazifanyia promotion nyimbo za B’Hitz huku mtu wa kwanza akiwa MRap lakini yeye alitoa masharti ya kuchagua wimbo wa kuanzia kufanyia promotion na kati ya nyimbo zote alichagua wimbo wa ‘Nishike’ ambao hata hivyo haukuwa chaguo la kwanza la MRap.
“Kwanza nilibahatika kuona wanavyotafuta chorus, yaani walishaingiza vocal wanatafuta chorus ya hiyo Nishike. Sasa nikiangalia naona sio tone ambayo wananchi wanaihitaji kwa sababu mimi niko karibu sana na wasikilizaji, nikasikiliza nikapata idea mwenyewe ya chorus nikaiandika my melody nikamwambia Pancho, Pancho akaniambia ‘yeah hii inafit kabisa’. nikampa kuna dogo mwingine ambaye alikuwepo ni rafiki yake huyo MRap ndio akampigia chorus. Mimi nikawa nimeondoka kabisa, ila baadae nilivyorudi nikaipitisha moja kwa moja ile nyimbo ndio nianze nayo kazi.” Ameeleza Shabani.

Kwa maelezo ya Shabaha kitendo cha yeye kuupitisha wimbo huo kuwa wa kwanza kutoka kulizua balaa baada ya muda kwa kuwa MRap hakupenda kabisa uamuzi huo.
“Baada ya kama siku mbili ikiwa inafanyiwa mixing, kwa sababu Hermy ndio alikuwa ameingia kwenye suala zima la kuifanyia mixing hiyo nyimbo, nikasikia yametokea matatizo, dogo amekwaruzana na Pancho.” Ameeleza Shabaha.
“Yeye dogo alikuwa kumbe hataki ile ngoma iende anataka iende nyingine kabisa, akawa sasa anampangia Pancho. Wakati muda huo mimi ndio nilikuwa nishaamua kuwa mimi ndio napanga…nishawaambia kabisa kuwa katika mkataba wangu mimi na ninyi cha kwanza kabisa tuwe tunakubaliana nini cha kufanya. Wote tukaeni tukubaliane na tupene sababu za msingi, mimi sasa nilikuwa nishakaa nao nikawapa sababu za msingi na hilo jambo likawa limepita. Kwamba ile nyimbo ndio inaenda. Ila dogo akawa anacrash kimpango wake.”
Ameongeza Shabaha ambaye anadai alikuwa ameshakula tenda ya kusambaza kazi za B’Hitz.
Kutokana na kutokukubaliana na wimbo huo ama kukubaliana kwa shingo upande na uamuzi Shabaha, MRap aliendelea kumpush Pancho Latino akimuuliza kuhusu wimbo wa Dedication ambao alitaka utoke na hapo ndipo ugomvi ulipoanzia na Pancho anadaiwa kushindwa kuvumilia kujirudia kwa ombi la MRap kuhusu wimbo ambao ulikuwa umempa kazi ya ziada ya kufanya wimbo mpya kwa haraka ili uanze kwenda hewani kwa masharti ya bwana Shabaha.




Baada ya kumalizana na bwana Shabaha, tovuti ya Times Fm ilimtafuta MRap kutaka kujua kwa upande wake kama ni kweli alikuwa anataka utoke wimbo tofauti na huo, na kama kweli huo ndio mzizi wa ugomvi kati yake na producer wa B’Hitz, Pancho Latino.


MRap alikiri kumfahamu bwana Shabaha na kueleza kuwa kweli alipewa hiyo kazi ya kuchagua na ndipo akachagua wimbo wa Nishike na kwamba kweli alikuwa anataka itoke Dedication.
“Eeh mimi nilikuwa nataka nitoe Dedication lakini kipindi kile niko B’Hitz, kwa hiyo mpaka nimemaliza mkataba wangu B’Hitz au kama sifanyi nao kazi hata mimi nilishaachana na zile nyimbo zote. Sasa sijui haya yote yanatoka wapi. Ilikatazwa kwamba walikuwa hawataki kutoa Dedication wakawa wanataka kutoa hii nyimbo inaitwa ‘Nishike’, then nikasema sawa.
“Sasa mpaka kutokuwa na maelewano kati yangu mimi na B’Hitz na Producer Pancho sasa mimi nikasema basi inabidi niendelee na mambo mengine ndo nikaondoka nikaenda AM Records nafanya kazi hapa na sehemu nyingine ambazo ntapewa beats na ntafanya kazi. Sasa haina maana kwamba mimi nazifikiria zile nyimbo hapana.” Ameeleza MRap.




Tovuti ya Times Fm ilitaka kufahamu kwa nini MRap alikuwa anaitaka zaidi ‘Dedication’ na sio wimbo mwingine wowote japo uongozi wake ulikuwa umeshauriwa tofauti.

“Mimi nilikuwa napenda… unajua ngoma ya Dedication ni ngoma ambayo niliwaahidi watu, unajua… the problem ni kwamba tulishaga anza kufanya promotion zamani katika mitandao Instagram nikasema ntaitoa siku ya Valentine then ikapita kwa sababu producer hakutaka itoke kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ana mipango yake ambayo mimi nilikuwa sijui. Kwa hiyo kama alishapanga usingeweza kumtoa kwenye huo mpango wake, kwa hiyo alivyosema Dedication hairuhisiwi kutoka nikasema basi watafanya watakavyo wenyewe.” Ameeleza MRap.
 
Kumekuwepo na taarifa kuwa MRap alikuwa tayari ameshafanya makubaliano na meneja wake wa zamani anayejulikana kama Wycliffe kuwa atoe wimbo wa ‘Dedication’ na sio wimbo mwingine ili wafanye biashara fulani kitu ambacho kilichochea nia ya MRap kuendelea kumsisitiza Pancho kuhusu Dedication japo tayari ilikuwa ishawekwa kando na mwisho ukazuka ugomvi mkubwa. Inawezekana kabisa hicho kilikuwa chanzo cha Pancho kughafilika na kufikia hatua ya kumpiga MRap kama alivyoeleza.

MRap amekiri kuwa kubadilika kwa mpango huo kati yake na meneja wake wa zamani kuliathiri mpango wake kwa kiasi fulani.
“Kuliniathiri kidogo lakini sasa hivi niko sawa kabisa, sina tatizo lolote. Hata ile nyimbo nikawa nimeacha tu kule basi tu fresh nikawa sina mpango nayo tena.” Amesema rapper huyo wa ‘Attention’.

Rapper huyo ameeleza kuwa alishaongea na uongozi wa B’Hitz na akawaomba msamaha kama kuna alichowakosea ili kila mmoja aendelee na mambo yake.

Mwisho MRap ameeleza kuwa ameubariki wimbo wa ‘Nishike’ na mashabiki wake waendelee kuudownload na kuusikiliza.

“Kwa sasa hivi ngoma ambayo nina uwezo wa kuipush ni Usinde Mbali ndio nyimbo ambayo ntakuwa nahangaika na ntaipush kadri ntakavyoweza kwa sababu ndio nyimbo ambayo nilianza nayo. Ila na hii nayo kwa sababu nilifanya mimi wanaweza kuwa wanaisikiliza kwa sababu it’s the same MRap, haina noma wala nini. Unajua we raping this music…good music kwa hiyo waendelee. Tupeane tu support na wanipe comments pia kwenye hiyo ngoma.”

Habari hii ni kwa hisani ya tovuti ya Times fm,unaweza kuingia ili usikilize live mahojiano hayo www.timesfm.co.tz

Post a Comment

Previous Post Next Post