Filamu ya Noah yashika nafasi ya kwanza kwenye Box Office, kukataliwa imekuwa sehemu ya 'kick'

Filamu ya ‘Noah’ iliyoigizwa na Russell Crowe iliyokataliwa katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu na Indonesia ni kama ilipewa ‘kick’ na hatua hiyo na kuwafanya watu waongeze hamu ya kuiona kitu ambacho kimeifaidisha zaidi katika wiki ya kwanza.

Filamu hiyo iliyotengenezwa kwa bajeti ya $130 milion, imemevuka kiwango kilichotarajiwa na waandaaji baada ya kuingiza pesa nyingi zaidi katika wiki yake ya kwanza kwenye Box Office na kushika nafasi ya kwanza kwa mauzo ya tiketi.
Kampuni ya Paramount Pictures ilikuwa imeweka matarajio ya kuuza tiketi za $30 million, lakini imeuza $44 million wikend hii.
Awali filamu hiyo ilileta mkanganyiko hasa wa kiimani katika simulizi lake linalotokana na simulizi halisi la Nuhu na gharika.
Mkanganyiko huo uliibuka baada ya kuonekana kuwa tofauti kati ya jinsi lilivyosimuliwa katika Biblia na Quran.
Hali hiyo iliwafanya nchi za Umoja wa Kiislamu kuipiga marufuku kwa maelezo kuwa ingewachanganya watu, lakini pia kwa imani ya kiislamu inakatazwa kumfananisha nabii na mtu wa kawaida kwa kuwa hali hiyo inaweza kuwafanya baadhi ya watu kumtukuza mtu huyo aliyevaa uhusika wa nabii.
Hii ni orodha ya filamu 10 zilizofanya vizuri zaidi wikendi hii kwenye Box Office:
   1.  Noah- $44.0 million
   2. Divergent - $26.5 million
    3. Muppets Most Wanted - $11.4 million
    4.  Mr. Peabody & Sherman" - $9.5 million
    5.  God's Not Dead - $9.1 million
    6.  The Grand Budapest Hotel" - $8.8 million
    7. Sabotage - $5.3 million
    8. Need for Speed - $4.34 million
    9. 300: Rise of an Empire - $4.3 million
    10.  Non-Stop - $4.1 million

Post a Comment

Previous Post Next Post