Floyd
Mayweather Jr
Mbabe anayetaraji
kuhitimisha zama zake A. Kusini
*Ni mwanamichezo anayeongoza kwa fedha, matumizi
LEO katika
maisha ya wenzetu tutakuwa na mbabe Floyd Mayweather Jr ‘Money’ anayetokea
katika ukoo wababe waliowahi kutikisa dunia kwa kutwaa ubingwa wa ngumi wa duniani
ambao ni baba yake mkubwa Floyd Mayweather Sr na baba zake wadogo, Jeff Mayweather
na Roger Mayweather.
Mbabe huyo
ambaye ametangaza kwa mara nyingine kwamba anamipango ya kucheza pambano lake
la mwisho Septemba 2015, nchini Afrika Kusini.
Bingwa huyo
aliyabainisha hayo wakati alipokuwa nchini Afrika kusini katika ziara yake ya
kutangaza mchezo huo nchini humo katika majimbo sita ikiwamo miji ya Bloemfontein, East London na Cape Town.
Bondia huyo
ambaye ni rafiki wa karibu wa rapper 50 Cent ana rekodi ya kushinda mara 45 na
hajawahi kupigwa hata pambano moja tangu aanze mchezo huo mwaka 1996, huku
akishinda kwa ‘KO’ (26).
Ujio wa
mwakani wa bondia huyo utakuwa wa pili baada ya ule wa kwanza ambao mbabe huyo
alifanikiwa kupewa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa utoaji wa tuzo wa
mwanamichezo bora wa mwaka wa Afrika Kusini.
USICHOKIJUA
Floyd
Mayweather amefuata nyayo za baba yake mzazi Floyd Mayweather aliyekuwa bingwa
wa dunia, baba yake mdogo Jeff Mayweather alikuwa bingwa wa uzito wa juu wa IBO
na baba yake mwingine, Roger Mayweather alikuwa bingwa wa dunia mara mbili,
kabla ya kuacha na kuwa kocha wa kijana huyo.
Ngumi za
ridhaa alizocheza takribani mapambano 84 yalimuwezesha Floyd, kung’aa na
kuonesha kipaji chake kutokana na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa nchini
Marekani ‘National Golden Gloves’ kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 1993, hadi
1996.
Floyd
kutokana na ugumu wake wa kutopigika, aliokuwa nao, wenzake walimpachika jina
la utani ‘Bitch Boy’ kutoka na usugu wa uso wake, uliokuwa hauchubuki wala
kuchanika akiwa ulingoni.
Sifa yake
kubwa ni ukwepaji wa makonde akifananishwa na enzi za baba yake, Floyd
Mayweather Sr na baba yake mdogo, Roger Mayweather, ambao ndio wamekuwa makocha
wake.
Baba yake
mdogo, Roger Mayweather alichukua jukumu la kumfundisha baada ya baba yake
mzazi, Floyd Mayweather Sr. kuhukumiwa kifungo jela baada ya kukutwa na dawa za
kulevya ndani ya gari lake mwaka 1993.
Baada ya
Mayweather Sr. kutoka jela alimchukua tena mwanawe na kumuendeleza kumfundiusha
na kumuwezesha kumshinda kwa KO, Sam Girard.
Mwaka 2006,
akiwa na miaka 29 pekee, Mayweather aliviita vyombo vya habari na kuvieleza nia
yake ya kutaka kustafu baada ya kucheza na Oscar De La Hoya.
Hatimaye Mei
5, 2007 pambano kati yake na bingwa wa WBC, Light Middle, De La Hoya na
kufanikiwa kushinda lakini alibatilisha uamuzi wake wa kustaafu ngumi.
FEDHA
Floyd
Mayweather anamiliki utajiri unaofikia kiasi cha dola milioni 216 (sawa na shilingi
milioni 216).
MATUMIZI YA FEDHA
Mbabe huyo ambaye ndiye mwanamichezo anayelipwa zaidi
amekuwa akielezwa kutumia fedha kwa fujo zaidi kuliko wanamichezo wengine,
kwani hata katika pambano lake lililopita la Septemba alilpwa kiasi cha dola
milioni 41.5.
Kutokana na matumizi yake makubwa ya fedha mbabe huyo
amepewa jina la utani la ‘Money’.
Tofauti na nyota wengine Mayweather amekuwa na mpambe anayebeba
mikoba ya mamilioni ya fedha katika matumizi yake na kulipa kwa fedha taslim
badala ya kulipa kwa hundi kama ilivyo kwa nyota wengine.
Hupendelea kuvaa viatu vya hali ya juu na hata nguo zake za
ndani amekuwa akivaa mara moja na kutupa.
Wapambe wake na hata wafanyabiashara zake wamepewa jina la
‘The Money Team’ alilalamikiwa kutumia fedha vibaya kiasi cha kutokuwa na fedha
benki hali iliyomfanya amuonesha mwandishi wa ESPN kitabu chake cha benki
kilichokuwa na dola milioni 123 na kumwambia kwamba hiyo ni akaunti moja tu
badoi nyingine.
Kwa kuonesha kwamba anatumia fedha kufuru mbabe huyo
alipokuwa katika moja ya ziara yake nchini Marekani alikuwa akitumia ndege
binafsi akiwa amempakia kinyozi wake pekee ingawa mara zote anakuwa amenyoa kipara
huku wapambe wake wengine akiwa amewakodia ndege nyingine.
Akiwa jijini New York alitumia karibu dola 250,000 (shilingi
miloni 400) kwa kununua vito vya mwanaye, Iyanna mwenye umri wa miaka 13
ambavyo ni Hereni na mikufu.
USAFIRI
Hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika ununuzi wa magari ambako
anaelezwa amekuwa akinunua magari ya kifahari mawili mawili kwa rangi tofauti
kwa nia ya kutumia katika majiji mbalimbali ya Marekani.
Inaelezwa kwamba kununua magari ya rangi tofauti yamekuwa
yakimuwezesha kutambua jiji analokuwa amefika kwa mfano anapokuwa Las Vegas
hutumia gari jeupe na anapokuwa Miami anatumia jeusi.
MAKAZI
Floyd
Mayweather anaishi Las Vegas katika jumba ambalo alilinunua na kulikarabati kwa
dola milioni 9. Jumba hilo lipo kwenye eneo lenye ukubwa wa futi za mraba
22,000. Vyumba vitano vya kulala, vyumba saba vya kuoga, baa ndogo, chumba cha
kuonea sinema, ukumbi wa mikutano, eneo la kucheza gofu, gereji.
WASIFU
JINA: Floyd
Mayweather Jr ‘Money’
UMRI: 37
KIMO: mita 1.73
UZITO: kilogramu 68
Makala hii imendaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mashirika
mbalimbali ya kimataifa
.DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION AMBAZO
ZINATARAJIWA KUWA HEWANI WIKI IJAYO NA MAPAMBANO YOTE YA NGUMI
YATAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO ZAIDI FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA
MSIMBAZI KARIAKOO PIGA SIMU 0713406938
Post a Comment