KAMPUNI ya magari ya General Motors
(GM) ya nchini marekani inatarajiw akutumia zaidi ya dola za marekani milioni
300 katika robo ya kwanza ya mwaka kwa ajili ya kufanyia marekebisho ya magari
yaliyokosewa kiufundi.
Kampuni hiyo imeyaita kiwandani
magari milioni 1.5 klatika awamu tatu tofauti.
Wito huo mpya ni mbali na ule wa
mwaka jana ambapo ulihusisha magari milioni 1.6 yaliyokosewa swichi za
kuwashia.
Magari milioni 1.18 ni pamoja nay
ale yaliyotengenezwa kati ya mwaka 2008 –
2013 aina ya Buick Enclave na GMC Acadia;
ya mwaka 2009 - 2013 aina ya Chevrolet Traverse na ya mwaka 2008 - 2010 aina ya
Saturn Outlook, ambayo yalikuwa na matatizo na Maputo ya kujiokolea ya pembeni
wakati wa ajali.
Pia kuna magari 303,000 aina ya Chevrolet
Express na GMC Savana ya kuanzia mwaka 2009 - 2014 yakiwa na uzito wa pauni
10,000 au chini yaliyo na tatizo upande wake wa juu.
Aidha yapo magari 63,900 aina ya Cadillac
XTS ya mwaka 2013 na 2014 yenye tatizo la joto na uwezekano wa kuzuka kwa moto
katika injini na kuungua kwa vifaa vilivyotengenezwa kwa plastiki.
Taarifa zaidi zinasema kwamba
kampuni hiyo ya GM inakabiliwa na
uchunguzi kwa namna ilivyoshughulikia kadhia hiyo ya kurejesha magari kiwandani
yenye tatizo la swichi linazloweza kuzuia puito kufanyakazi yake wakati wa
ajali.
Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Mary
Barra amesema kwamba amewaambia wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhakikisha kwamba
wanafanyakazi kwa uaminifu nna kasi kurekebisha matatizo yaliyojitokeza.
Post a Comment