AZAM FC na Yanga zimekutana mara 11
kwenye ligi kuu, Yanga ikiwa imeshinda michezo mitano, huku Azam FC
ikishinda michezo minne na michezo miwili zikitoka sare.
Nje ya ligi kuu zimekutana mara tano,
Yanga ikishinda mara mbili (Ngao ya Hisani na Kagame Cup na Azam FC
ikishinda mara tatu (Mapinduzi Cup na mechi za kirafiki)
Kiujumla Azam FC na Yanga SC zimekutana
mara 16 Yanga ikishinda mara saba na Azam FC ikishinda mara saba pia
huku michezo miwili timu hizo zikitoka sare.
Tathmini hii inaonesha kuwa timu hizi
zina nguvu sawa, yeyote anaweza kushinda mchezo wa leo ambapo timu hizi
zinakutana mara ya 17,Je nani atashinda?
John Bocco anaendelea kuwa mchezaji
aliyefunga magoli mengi zaidi huku Nadir Haroub Canavaro akiwa mchezaji
aliyecheza mechi nyingi zaidi kati ya Azam FC na Yanga.
Yanga inatoka Kariakoo Ilala DSM, wakati
Azam FC inatokea Mbande Temeke DSM, Huwezi kuita mechi hii Derby maana
inakutanisha timu ambazo hazitoki eneo moja… Lakini ubora wa mechi kati
ya Azam FC na Yanga umeendelea kukua kila kukicha na bila shaka tunaweza
kuliita pambano hili Classic Game… au El Classical
Azam TV itawaletea mtanange huu live kupitia chaneli yake ya Azam Two kuanzia saa kumi kamili jioni ya leo
Mungu Ibariki Azam FC… Mungu wabariki wachezaji wa Azam FC waweze kuibuka na ushindi
CHANZO: TOVUTI YA AZAM FC
Post a Comment