Viongozi wakuu wa kampuni ya Smart Telecom,Afrika Masharikii
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi waliojipatia zawadi
kupitia mtandao huo,baada ya kushiriki kwenye kampeni ya GIVE US A NAME
iliofanyika hivi karibuni.
Pichani
kati ni Balozi wa Kampuni hiyo ya simu iliyozinduliwa leo jijini
Dar,Msanii wa maigizo ya vichekesho atambulikae kwa jina la Hemed
Maliyaga a.k.a Mkwere Orijini akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Telecom,Afrika Mashariki,Abdullatif Bouziani (shoto) na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham wakiwa katika picha ya pamoja.
Afisa
Mtendaji MKuu wa Smart Telecom,Afrika Mashariki,Abdullatif Bouziani
akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye
uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar,kulia kwake
ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham
Pazia likishushwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kampuni hiyo ya simu za mikononi-Smart."lets talk.
Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom,Afrika Mashariki,Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar
IPS kukuza ujasiliamali wa jamii katika mawasiliano ya simu
Burundi, Uganda na Tanzania
Machi
19, 2014 Shirika la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya
viwanda chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED),jana wametangaza
kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini ya kampuni iitwayo
SMART.
Jina la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika
kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED kukuza
huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda, lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja
Mtandao
wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni washirika
wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma za mawasiliano
nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika shirika la Tcell linaloongoza
katika kutoa huduma Tajikistan.
IPS pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee
waliowekeza SEACOM submarine cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao
ushirika wa IPS ndani ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya
ushirikiano wa makampuni ya simu Nepal na Cambodia na kuwafanya wawe waongozaji katika soko hili.
Kuzinduliwa kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa
AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi
wa sauti ambao utatoa fursa nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika
Mashariki. AKFED imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance
Group, National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na
miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.
“Kazi zetu katika mawasiliano kwa njia ya simu
hasa Roshan-Asia ya kati ni kuboresha uwekezaji wa jamii katika miundombinu ya
jamii, huduma za afya na elimu. Pia kutengeneza biashara yenye mafanikio katika
soko ili tuweze kujitofautisha na washindani wengine, Tunatazamia kuwa
uwekezaji katika kampuni dada ya AKDN utakua umeenea katika nchi za Burundi,
Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka 100” alisema Lutaf Kassam Meneja wa IPS
SMART itaingia katika masoko haya ikiwa na
dhamira ya embrance tamaduni za ndani ili kuboresha jamii wanakofanyia
kazi.mfano mzuri wa dhamiri hii ni njia ambayo jina la kampuni
lilivyochaguliwa. Kampeni ya Tupe Jina ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2013
ikiwahamasisha watu wa Afrika Mashariki kupendekeza na kulipigia kura jina la
kampuni.
Kampeni hiyo iliwavutia zaidi ya watu 70,000 na majina tofautitofauti
yalipendekezwa na kupigiwa kura. Mwisho kampeni ililipata jina la SMART
ikikusudia kuangalia uvumbuzi wa mawazo katika soko la Afrika Mashariki.
Post a Comment