Gharama ya chakula pia imepanda
Utafiti mpya nchini Kenya
umeonyesha kuwa idadi kubwa ya wakenya wanakerwa zaidi na hali ya
mfumuko wa bei na gharama ya juu ya maisha kuliko kitu kingine chochote.
Wasiwasi unaokuja baada ua mfumuko wa bei ni
ukosefu wa ajira. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya
utafiti kuhusu maswala ya kijamii na kisiasa IPSOS Synovate.Baadhi wanaona kuwa hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 haitazaa matunda kwani bado kuna changamoto ya ufisadi na uharibifu wa pesa za serikali.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 81 ya waliohojiwa walisema kuwa wanategemea huduma ya matibabu katika hospitali za umma ambazo zinakabiliwa na changamoto za vifaa.
Nini kero kubwa zaidi nchini mwako, je ni siasa, gharama ya maisha, ni nini hasa kinachokera? Toa jibu lako kwa ukurasa wetu wa Facebook Bofya http://goo.gl/U5iUvg

Post a Comment