M-Rap alijiondoa B’Hitz kabla ya mkataba kuisha, mtu aliyekabidhiwa kusimamia promotion yake aongea

m,rapTofauti iliyojitokeza kati ya rapper M-Rap na B’Hits Music Group imechukua sura mpya baada ya kudaiwa kuwa mkataba wa M-Rap na studio hiyo haukuwa umeisha kama rapper huyo anavyodai na kwamba alikuwa akitaka kuachia wimbo tofauti na ule kampuni ilikuwa imeafikiana kuutoa.
B’Hits wanadai walitafuta mtu maalum aitwaye Shabaha atakayekuwa anasimamia shughuli ya promotion ya nyimbo za wasanii wake na msanii wa kwanza kufanyiwa hivyo alikuwa M-Rap. “Kwanza nilibahatika kuona wanavyotafuta chorus, yaani walishaingiza vocal wanatafuta chorus ya hiyo ya Nishike,” Shabaha ameiambia tovuti ya Times FM.
“Sasa nikiangalia naona sio tone ambayo wananchi wanaihitaji kwa sababu mimi niko karibu sana na wasikilizaji, nikasikiliza nikapata idea mwenyewe ya chorus nikaiandika my melody nikamwambia Pancho, Pancho akaniambia ‘yeah hii inafit kabisa’. nikampa kuna dogo mwingine ambaye alikuwepo ni rafiki yake huyo MRap ndio akampigia chorus. Mimi nikawa nimeondoka kabisa, ila baadae nilivyorudi nikaipitisha moja kwa moja ile nyimbo ndio nianze nayo kazi,”
aliongeza.
“Baada ya kama siku mbili ikiwa inafanyiwa mixing, kwa sababu Hermy ndio alikuwa ameingia kwenye suala zima la kuifanyia mixing hiyo nyimbo, nikasikia yametokea matatizo, dogo amekwaruzana na Pancho. Yeye dogo alikuwa kumbe hataki ile ngoma iende anataka iende nyingine kabisa, akawa sasa anampangia Pancho. Wakati muda huo mimi ndio nilikuwa nishaamua kuwa mimi ndio napanga…nishawaambia kabisa kuwa katika mkataba wangu mimi na ninyi cha kwanza kabisa tuwe tunakubaliana nini cha kufanya. Wote tukaeni tukubaliane na tupene sababu za msingi, mimi sasa nilikuwa nishakaa nao nikawapa sababu za msingi na hilo jambo likawa limepita. Kwamba ile nyimbo ndio inaenda. Ila dogo akawa anacrash kimpango wake.”
Tovuti hiyo imeandika kuwa kutokana na kutokukubaliana na wimbo huo ama kukubaliana kwa shingo upande na uamuzi Shabaha, M-Rap aliendelea kumshinikiza Pancho Latino kuhusu kuachia wimbo uitwao Dedication na hivyo kupelekea kuzuka ugomvi kati ya wawili hao kwakuwa tayari maamuzi yalikuwa yamepitishwa ya kutoa wimbo mwingine.
“Eeh mimi nilikuwa nataka nitoe Dedication lakini kipindi kile niko B’Hitz, kwa hiyo mpaka nimemaliza mkataba wangu B’Hitz au kama sifanyi nao kazi hata mimi nilishaachana na zile nyimbo zote. Sasa sijui haya yote yanatoka wapi. Ilikatazwa kwamba walikuwa hawataki kutoa Dedication wakawa wanataka kutoa hii nyimbo inaitwa ‘Nishike’, then nikasema sawa,” M-Rap ameiambia tovuti hiyo.
“Sasa mpaka kutokuwa na maelewano kati yangu mimi na B’Hitz na Producer Pancho sasa mimi nikasema basi inabidi niendelee na mambo mengine ndo nikaondoka nikaenda AM Records nafanya kazi hapa na sehemu nyingine ambazo ntapewa beats na ntafanya kazi. Sasa haina maana kwamba mimi nazifikiria zile nyimbo hapana,”
aliongeza.
M-Rap anadai kuwa kung’ang’ania kutoa ‘Dedication’ kulitokana na kutaka kutimiza ahadi aliyotoa kwa mashabiki wake.
“Unajua ngoma ya Dedication ni ngoma ambayo niliwaahidi watu, unajua… the problem ni kwamba tulishagaanza kufanya promotion zamani katika mitandao Instagram nikasema ntaitoa siku ya Valentine then ikapita kwa sababu producer hakutaka itoke kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ana mipango yake ambayo mimi nilikuwa sijui. Kwahiyo kama alishapanga usingeweza kumtoa kwenye huo mpango wake, kwa hiyo alivyosema Dedication hairuhisiwi kutoka nikasema basi watafanya watakavyo wenyewe,” alisema rapper huyo.
Tovuti hiyo imedai kumekuwepo na taarifa kuwa M-Rap alikuwa tayari ameshafanya makubaliano na meneja wake wa zamani, Wycliffe kuwa atoe wimbo wa ‘Dedication’ na sio wimbo mwingine ili wafanyebiashara ‘fulani’ kitu ambacho kilichochea nia ya M-Rap kuendelea kumsisitiza Pancho kuhusu Dedication japo tayari ilikuwa ishawekwa kando na mwisho ukazuka ugomvi mkubwa.
Hata hivyo M-Rap ambaye aliiambia Bongo5 kuwa hautambui wimbo wake ‘Nishike’ uliotolewa na B’Hits, amebadilisha msimamo na sasa anautambua.
“Kwa sasa hivi ngoma ambayo nina uwezo wa kuipush ni Usinde Mbali ndio nyimbo ambayo ntakuwa nahangaika na ntaipush kadri ntakavyoweza kwa sababu ndio nyimbo ambayo nilianza nayo. Ila na hii nayo kwa sababu nilifanya mimi wanaweza kuwa wanaisikiliza kwa sababu it’s the same M-Rap, haina noma wala nini. Unajua we raping this music…good music kwahiyo waendelee. tupeane tu support na wanipe comments pia kwenye hiyo ngoma,”
alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post