
Wizara ya usafiri ya Malaysia
inasema kuwa imeomba ushirikiano wa nchi zote kwenye njia mbili ambapo
ndege iliyopotea juma lilopita huenda kuwa imepita.
Imeomba msaada wa data kutoka Satelite na Radar na msaada katika shughuli za msako.Polisi wa Malaysian wanasema piya wanachunguza historia ya wafanyakazi wengine wa ndege na abiria wote pamoja na wahandisi waliohudumia ndege hiyo.
Waziri wa Usafiri, Hishammuddin Hussein, alisema sasa nchi 25 zimehusika katika msako.
Alisema sasa wanalenga zaidi njia mbili ambazo pengine ndege hiyo ilifuata - kaskazini au kusini.
Post a Comment