MBUNGE MAARUFU WA CHADEMA AFUNGUKA ON MUUNGANO LIVE!!

 
·
Tunataka nini?

Tunataka kujenga Tanzania kama Taifa moja lisilo na ubaguzi wa aina yeyote na lenye kutumia utajiri wa nchi kutoa fursa kwa watu wake wote kustawisha maisha yao. Waasisi waliweka misingi imara ya Taifa moja, Nchi moja na Dola moja. Wale wanaotaka kubomoa misingi hii hawana nafasi. Wale wanaotaka tuvunje Nchi yetu, tuvunje vunje Taifa letu na kuporomosha dola yetu watafute Nchi nyingine. Dola zinajengwa, hazibomolewi.

 
Tunapotaka tuwe na muundo Mpya wa Muungano sio kwamba tunataka kuunda vidola vidogo viwili vya Tanganyika na Zanzibar. La hasha. Tunataka kuibakizia Dola yale mambo ya msingi ya kiDola na Serikali za Washirika kutekeleza mambo ya kila siku yanayohusu wananchi. Hakuna mshirika yeyote wa Muungano wa Tanzania mwenye kuweza kuwa na 'Nation State' maana mazingira hayo hayapo Tanzania. Wakuu wa Serikali za Washirika watakuwa na madaraka kamili katika maeneo hao na Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu atakuwa na mamlaka kamili kwa Jamhuri ya Muungano.
Nimeandika katika kumbukumbu zangu maneno haya
Muungano imara wa Serikali Tatu
"Kila mtu sio Mwalimu Julius Nyerere. Kila mtu sio Sheikh Abeid Amani Karume. Kuna watu dhaifu na dhalili wenye uchu wa madaraka ambao wakikabidhiwa kuongoza Serikali za Washirika watajinyakulia mamlaka makubwa. Tunachotaka sasa ni Serikali ya Muungano iliyo imara, iliyo na uzalendo usiotia shaka, Serikali yenye nguvu ya kuiweka nchi pamoja kwa namna yeyote ile bila kujali lolote"

Post a Comment

Previous Post Next Post