
Mgombea
Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu
Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na mmoja wa wanakijiji,mara baada ya
kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo wa jimbo
hilo,uliofanyika katika kijiji cha Wenda kata ya Mseke-Iringa
Vijijini,huku kukiwa na mvua kubwa ikinyesha,ambayo hata hivyo haikuzuia
kufanyika kwa mkutano huo.Wananchi wa Kijiji hicho walionekana kuw ana
shauku kubwa ya kutaka kumsikiliza Mgombea huyo bila kujali kulowana na
mvua.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16.

Wanakijiji
cha Wenda wakimpungia Mgombea Ubunge wa CCM,jimbo la Kalenga,Ndugu
Godfrey Mgimwa,huku shangwe na vifijo vikiwa vimetawala eneo hilo pasina
kujali mvua kubwa ilioyokuwa ikiendelea kunyesha eneno hilo.


Pamoja na Mvua kubwa iliyokuwa inanyesha katika kijiji
cha Wenda kata ya Mseke-Iringa Vijijini,wanakijiji wa eneo hilo
walionekana kuvutiwa mno na sera za mgombea ubunge wa CCM,Godfrey Mgimwa
alipozungumza nao kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Kama uonavyo
pichani baadhi ya Wanakijiji wakilikimbiza gari ya mgombea huyo mara
baada ya kumaliza mkutano wake.Mgombea huyo aliwaomba wampigie kura za
ndio na kumpa ridhaa ya kuwaongoza kama Mbunge wa jimbo hilo,ili
wayamalizie yale yaliyokuwa yameachwa na Mbunge aliyekuwepo hapo
awali,Marehemu Dk Willliam Mgimwa.
Post a Comment