Ndege nyingine ya Malaysia Airlines yatua Hong Kong kwa dharula baada ya kupata hitilafu ya umeme

malaysia airlinesWakati bado juhudi zinaendelea bila mafanikio za kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines aina ya Boeing 777-200 iliyopotea March 8 mwaka huu ikiwa na abiria 239, ndege nyingine ya shirika hilo imelazimika kutua Hong Kong, china kwa dharula baada ya hitilafu za umeme kujitokeza ikiwa safarini.
Maafisa wa shirika hilo wameiambia CNN mapema leo kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A330-300 iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur kuelekea Incheon, Korea Kusini ililazimika kubadili njia na kwenda kutua kwa dharula Hong Kong baada ya wafanyakazi wa ndege hiyo kugundua hitilafu katika genereta inayozalisha umeme wa kawaida wa ndege hiyo.
Kuala Lumpur ndio uwanja wa ndege ilipotokea ndege ya shirika hilo iliyopotea ambayo hadi sasa bado haijaonekanekana.
Hata hivyo maafisa hao wameongeza kuwa pamoja na hitilafu iliyojitokeza lakini umeme uliendelea kuzalishwa kupitia power unit ndogo ya ndege hiyo.
SOURCE: MAIL ONLINE

Post a Comment

Previous Post Next Post