HIVI aribu karibuni wajumbe 629 wa Bunge Maalumu la Katiba. Wamejiweka
kitanzi na kuagana na Mungu kutenda haki watakapopitia na kuiboresha
Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo
Jaji Joseph Sinde Warioba.
Nasema wamejifunga Kitanzi kwa sababu wamefanya Agano naye Agano la Utii
kwake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama lilivyokuwa Agano la
Mwanaye Yesu Kristo kuwa, la kumpendeza Mungu na Watu. Je Wabunge wa
Katiba watalitimiza agizo hilo?
Lakini Yesu alilitimiza Agizo! Biblia inasema, “Yule mtoto akakua,
akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na
wanadamu Luka 2:40, 50.
Mwishoni mwa wiki; Niliwasikia Wabunge wa Bunge Maalum mjengoni kwa
majina yao, wakimwomba Mungu kwa majigambo wakitaka awasaidie kupitia
vitabu vyake vitakatifu vya Biblia na Kurani, na hiki ndicho kiapo
chao;-
“MIMI… [Jina la Mjumbe]…niliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge Maalumu,
naapa/ nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza
wajibu wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo, na bila
kukiuka sheria za nchi. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.”
Sasa ninavyomfahamu Mungu na jinsi ambavyo wengi wetu husema sauti Wengi
ni ya Mungu, hata kama humo ndani ya uteuzi kulikuwa na Mkono wa Mtu
kupendelea Chama au Asasi na Taasisi yake, mradi Mungu ameombwa asaidie,
uharifu ule unatakaswa na anakuita yeye kufaya kazi yake kwa ajili ya
watu si Jakaya Kikwete.
Baada ya Toba ile iliyofanywa kwa Biblia na kumtaja, anaingilia kati na kutoa Wito wake huu,
“Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, …[Jina la Mjumbe]……..
..yeye aliyekuumba, Ee Israeli,….[… …[Jina la Mjumbe]…….. asema hivi,
Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
“Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito,
haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto
hautakuunguza”. Isaya 43:1-2 unaitwa hivyo Mungu si Kikwete tena ili
uitende kazi yake kwa ajili ya watanzania ambao ni watu wake.
Sasa ikifika mahali mtu aliyeitwa kwa wito huo wa Mungu baada ya kufutwa
wito wa Kikwete, ambao pengine ndani yake tunasema kulikuwa na Hati ya
Mashitaka na Hukumu….yaani…
“Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake,
iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea
msalabani;
Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri,
akizishangilia katika msalaba huo” Kolosai 2:14-15 halafu anatokea mtu
anafanya madudu humo bungeni, Kitakuwa kilio na watu wanaweza wakaehuka,
wakapoteza viungo au kufa, maana ataona amedharauliwa.
Biblia inasema hivi, “Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka
mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye
atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake”. Kitabu cha
Kwanza cha Wafalme 2:10.
Hivyo nawasihi sana Wabunge wa Bunge Maalum wasijaribu kumuuthi Mungu
ili hali wamemuomba kwa vitabu vyake na kukiri kuwa watatenda haki
halafu wakakiuka, maana Ushahidi wa hati ya Mashitaka na Hukumu yenu ni
ukiri kupitia vitabu hivyo.
Kwa nyakati fulani tumeshuhudia Viongozi wa Siasa katika Vyama na
Serikali, wamekuwa wakiapa na wakikiri kwa kiapo hicho, lakini baada
wanapoenda kuwatumikia wananchi wamekuwa wanafaanya tofauti na tukaona
walivyofanywa!.
Wengine wamepoteza Maisha, Viungo, Nyadhifa zao, Familia zao, kwa Ajali
na Ulemavu mbalimbali na kudhani ni Mikosi kumbe wamesahau, katika kiapo
walichomuapia Mungu kufanya, na wamekikiuka.
Humo bungeni mnao wachungaji na waombaji, na huku nje wako waombaji
ambao wengine wanafunga na kuomba hadi mwisho wa Bunge hilo, hivyo ni
rai yangu msithubutu kuleta utoto kama ule wa Posho na mMengine ya
kuchelewsha Muda. Kwaherini
Chanzo: chademadiaspora.blog
Post a Comment