Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe
na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini, Dkt
Frank-Walter Steinmeier wakiwasili kwenye chumba cha mkutano kuzungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
SERIKALI
ya Ujerumani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imeahidi kutumia
zaidi ya Euro milioni 10 kukarabati reli ya kati (Central Line Railway).
MOblog inaripoti.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ujerumani nchini, Dkt Frank-Walter Steinmeier, Waziri wa Mambo ya Nchi
za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe amesema serikali
ya Ujerumani imekubali kwa dhati kabisa kukarabati reli ya kati kwa
manufaa ya Tanzania na nchi jirani.
“kwa
sasa siwezi kusema ukarabati utaanza lini na jina la mwekezaji kwa
sababu mazungumzo yanaendelea lakini kwa hakika kabisa tumeshakubaliana
kwenye jambo la ukarabati wa reli ya kati,” amesema Waziri Membe
Amesema
reli ya kati itapunguza matumizi ya barabara kwa mizigo na barabara za
nchi zitakuwa salama na kuongeza tija katika Nyanja za biashara kupitia
soko la pamoja Afrika Mashariki na kati.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza
waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea
mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Membe
alilisisitiza kwamba ziara ya Waziri mpya wa mambo ya nje kutoka
Ujerumani ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa sababu amekuja na
wawekezaji 65 kutoka maeneo mbalimbali.
Amesema
kuwa ukarabati wa reli ya kati ni muhimu katika kudumisha ushirikiano
wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili kwa maslahi ya watu wao.
“reli
ya kati kama mnavyojua ilijengwa na Wajerumani mwaka 1913 na kwa sasa
ina miaka karibu mia moja na kitu,” aliongeza Waziri Membe
Kwa
upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Steinmeier
amesema kuwa nchi yake itaendelea kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na
kijamii na Tanzania katika jitihada za kuharakisha maendeleo ya nchi na
watu wake.
Amesema
kuwa serikali ya Ujerumani imeamua kukarabati reli ya kati katika
jitihada za kukumbuka na kudumisha historia ya muda mrefu kati ya nchi
hizo mbili.
“najisikia furaha na faraja kuona nchi yaTanzania inapiga hatua mbele kimaendeleo baada ya uhuru wake,” amesema
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa kihistoria na
kiuchumi kati ya Tanzania na Ujerumani jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani nchini.
Sehemu ya waandishi wa habari nchini pamoja na waandishi kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo leo jijini Dar.
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Waziri Membe na mgeni wake wakiondoka kwenye chumba cha mkutano kuelekea Ikulu kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Post a Comment