Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, shabiki mmoja wa timu ya Azam FC amefariki
dunia jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati timu
hiyo ilipokuwa inacheza na timu ya Yanga.
Shabiki huyo alizimia uwanjani mara baada ya Yanga kupata bao lake la
kwanza lililofungwa na Didier Kavumbagu. Hata hivyo wasamaria wema
walimbeba shabiki huyo na kisha kuwekwa kwenye machela na kupelekwa
katika vyumba vya huduma ya kwanza.
Muda mchache baadae vipaza sauti vya Uwanja waTaifa vilisikika
vikitangaza kwamba kuna mtu amezimia na kama kuna ndugu au mtu yoyote wa
karibu na mtu huyo ajitokeze. Taarifa zimeeleza kuwa mtu huyo amefariki
akiwa katika chumba cha huduma ya kwanza.
Katika mchezo huo ambao Yanga walianza kupata bao katika kipindi cha
kwanza dakika ya 14. Hata hiyvo Azam ilipambana vikali na kurudisha bao
katika kipindi cha pili ikiwa ni dakika ya 82 wakiwa wachezaji kumi
baada ya Erasto Nyoni kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana
muamuzi.
Taarifa zaidi sikiliza hapa.
Taarifa zaidi sikiliza hapa.
Post a Comment