Meneja
wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael akiwakabidhi msaada
wa vitabu, Happiness Mathias (kushoto) na Ibrahim Issa, wanafunzi wa
shule ya Kilimani, iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam mapema jana.
Akishuhudia katikati yao ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Zubeda Jeni.
Tigo ilikabidhi msaada wa vitabu 905 vyenye thamani ya milioni 6.1 na
tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 kwa shule hiyo.
Mratibu
wa Elimu wa kata ya Manzese Bi. Petronila Liyamuya (kulia) akipitia
moja ya vitabu vilivyokabidhiwa na Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii
kutoka Tigo Woinde Shisael (kushoto) katika shule ya msingi Kilimani,
Manzese. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Kilimani Bi. Zubeda
Jeni.
Katika
jitahada za kusaidia kuboresha hali ya maisha ya watanzania kupitia
kuwekeza katika mipango ya maendeleo ya kijamii, Tigo Tanzania leo
imetoa msaada wa vitabu vya wanafunzi wa darasa la nne hadi la saba
vyenye thamani ya shilingi milioni 6.1/- kwa shule ya msingi Kilimani
iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi
msaada huo katika shule hiyo, Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Tigo,
Woinde Shisael, alisema kwamba kampuni hiyo ya simu inatambua fika
umuhimu wa elimu kama kiungo muhimu katika kuchangia mabadiliko kwenye
jamii na taifa kwa ujumla.
Woinde
pia alikabidhi, tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 4,000 za
maji la thamani ya shilingi 653,000/-, pesa iliyokusanywa kutoka kwa
wafanyakazi wa Tigo. Alisema msaada huo utachangia kuboresha mazingira
bora yakujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na walimu shuleni hapo.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya Kilimani iliyopo Manzese Bi. Zubeda Jeni (kushoto)
akimshukuru Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael
kwa msaada wa tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 yenye thamani ya Tsh
653,000/- pesa iliyochangishwa na wafanyakazi wa Tigo.
“Kama
inavyoeleweka kwamba elimu ni ufunguo wa maisha ya mtu, jamii na hata
taifa zima kwa ujumla, ndio sababu Tigo inapenda kutoa msaada huu kwa
wanafunzi wa shule hii ili kuwawezesha kutimiza ndoto hii,” alisema
Shisael.
Ukiondoa
sekta ya elimu, Tigo pia inasaidia sekta zingine za kijamii zikiwemo
afya, kutengeneza ajira na ujasiriliamali jamii, mipango ambayo kwa
mujibu wa Shisael imeweza kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania
nchi nzima.
Akipokea
msaada huo, mwalimu mkuu wa shule hiyo Zubeda Jeni, aliishukuru Tigo
kwa msaada huo akisema kwamba msaada wa vitabu hivyo utasaidia kuinua
kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
“Tunapenda
kuwashukuru Tigo kwa msaada huu ambao tunaamini utasaidia kwa kiasi
kikubwa wanafunzi na walimu katika kutimiza malengo yao ya kufaulu
vizuri katika mitihani yao,” alisema Jeni.
Risala
ikisomwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kilimani Bi. Zubeda Jeni ambapo
aliishukuru kampuni ya simu Tigo kwa msaada wa vitabu na tenki la maji
iliyotolewa. Mwalimu mkuu huyo alisema msaada huo uliotolewa ni kitendo
cha kizalendo kilichofanywa na anaamini kwamba vitabu hivyo vitaongeza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi walio darasa la nne na la saba
wataonufaika moja kwa moja na msaada huo.
Wafanyakazi
wa Tigo katika picha ya ukumbusho na wanafunzi na walimu wa shule ya
Kilimani iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam. Tigo ilifika mapema jana
kutoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 6.1 pamoja na
tenki la kuhifadhia maji yenye uwezo wa kubeba lita 4000.
Wanafunzi wa
darasa la nne na la saba wa shule ya msingi Kilimani wakiimba wimbo wa
“Tanzania, Tanzania” kama ishara ya uzalendo na kutambua mchango wa Tigo
kama kitendo cha kiungwana kwa shule hiyo.
Post a Comment