
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akisoma taarifa
ya tume mbele ya waandishi wa habari inayohusu ufafanuzi kuhusu daftari
la kudumu la wapiga kura litakalotumika katika uchaguzi wa ubunge
jimbo la Kalenga,kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Himid Mahamoud Himid na upande wa
kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba.

Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akibadilishana
mawazo kabla ya kujibu swali kwa waandishi wa habari ambao waliuliza
kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na daftari la kudumu na Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Himid Mahamoud Himid.
Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Himid Mahamoud Himid.

Kamishna
wa Tume ya Uchaguzi Jaji John Joseph Mkwawa akizungumzia suala zima la
vyama kuwa makini siku ya kupiga kura kwani hakutotakiwa kuwe na alama
ama kielelezo cha chama fulani katika siku hiyo,kushoto kwake ni Profesa
Amon Chaligha .

Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akijadiliana suala la
takwimu za daftari la kupiga kura pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndugu
Julius Malaba na Dk.Sist Cariah Naibu Katibu wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura na Tehama ambapo wapiga kura ambao taarifa zao zimetokea
zaidi ya mara moja waliondolewa kwenye daftari hilo na ni wapiga kura
hao kwa idadi ni 142.

Baadhi
ya maofisa wa Tume ya Uchaguzi wakisikiliza kwa makini kikao cha Tume
ya Uchaguzi na Waandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa juu ya
daftari la kudumu litakalotumika kwenye uchaguzi wa ubunge Kalenga siku
ya tarehe 16 Machi 2014 ambapo taarifa za uhakiki zilizofanyika
zilikuwa 149 tu na wapiga kura walioongezeka katika daftari
lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 ni 7 tu na sio 600 kama
ilivyoripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari.Picha na Adam Mzee
Post a Comment