Hadidu rejea
1) Kuchunguza uendeshaji wa mkataba wa kuzalisha Umeme kati ya kampuni ya IPTL na TANESCO
2) Kuchunguza
kama wakati escrow inafunguliwa kampuni ya mechmar ilikuwa inamiliki
IPTL, kama ilikuwa imefilisiwa na kama ilikuwa imehamisha umiliki wake
kwa kampuni ya PAP.
3) Kuchunguza na kuthibitisha ushahidi wa kampuni ya PAP kununua kampuni ya mechmar na kumiliki IPTL
4) Kuchunguza
chanzo cha mgogoro kuhusu tozo kati ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha
ushahidi wowote kuwa mgogoro uliamuliwa kwa faida ya IPTL
5) Kuchunguza
kama ilikuwa sahihi kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kusamehe kodi ya
VAT ya jumla ya tshs 26 bilioni kutokana na tozo ya capacity charges na
TRA wachukue hatua gani kuhakikisha kodi hiyo inakusanywa
6) Kuchunguza
kiwango cha fedha kilichopaswa kuwemo katika akaunti ya escrow, kiwango
gani kilikuwepo wakati IPTL wanalipwa na kiwango gani kitapaswa kulipwa
zaidi kutoka tanesco
7) Kuchunguza
madai ya benki ya standard chartered kwa tanesco na madai mengine
yeyote yanayohusiana na mkataba wa kuzalisha Umeme wa IPTL na iwapo
Serikali imejihadhari na uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa,
nafasi na heshima ya nchi katika kuheshimu mikataba ya kimataifa na ya
uwekezaji.
8) Kuchunguza
iwapo Wizara ya Nishati na madini ambayo ni mhusika Mkuu wa akaunti ya
tegeta escrow ilifanya ‘due diligence’ ya kutosha kabla ya kuingia
makubaliano ya kutoa fedha zilizopo akaunti ya tegeta escrow. Kupata
Maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na madini ni kwa nini aliagiza
ukaguzi maalum wakati yeye ni mhusika Mkuu kwenye mchakato mzima na
ilhali akijua PAC tayari imeanza mchakato wa ukaguzi.
9) Kutoa
mapendekezo ya njia bora za kisheria kulinda Taifa kutoingia hasara
zaidi katika mkataba wa IPTL chini ya wamiliki wapya
10) Kutoa
ushauri kwa kamati ya PAC juu ya mapendekezo ya hatua ambazo Bunge
linapaswa kuchukua kuhusu matokeo ya ukaguzi huu maalumu
Imetolewa na;
KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
Post a Comment